Lowassa afunguka kuhusu Rais Samia, ampa tano kwa kujenga uchumi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ya kujenga uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Lowassa ametoa pongezi hizo leo Septemba 24, 2021 kupitia ujumbe maalum aliouandika.

"Kwanza nianze kwa kumpongeza na kumshukuru Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya vyema kazi ya kuijenga nchi na kisha kuendeleza safari ya kujenga uchumi imara.
"Kupitia hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Marekani jana Alhamisi, Mama Samia amelirejesha tena taifa letu katika ramani ya Dunia.Katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani, Rais Samia amefanikiwa kuanza kujenga imani ya sekta binafsi katika kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi.

"Safari ambayo hatuna budi sote kumuunga mkono na kumsaidia, ili aliwezeshe taifa kuwa imara zaidi kiuchumi na kuiweka nchi katika utawala wa sheria.

"Rais Samia amethibitisha pasi na shaka kwamba Tanzania imepata nyota ya jaha kwa kuwa na kiongozi mkuu mwanamke hodari na shupavu ambaye leo hii tuna kila sababu ya kujivunia na kumuunga mkono,"amefafanua Mheshimiwa Lowassa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news