Mapokezi ya uchanjaji chanjo ya UVIKO-19 Awamu ya Pili yashika kasi Lushoto

Na Yusuph Mussa, Lushoto

ZOEZI la uchanjaji Awamu ya Pili ya ugonjwa wa UVIKO 19 linakwenda vizuri katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, kwani tangu uchanjaji huo umeanza rasmi Septemba 27, mwaka huu, watu wanaongezeka siku hadi siku.
Mwananchi wa Kijiji cha Gare, Kata ya Gare maarufu kwa jina la Mapichapicha akipata chanjo ya UVIKO-19 kutoka kwa Afisa Muuguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Veronica Shehiza, huku akichati na simu. (Picha na Yusuph Mussa).

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Septemba 30, 2021, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Lucy Maliyao alisema hadi Septemba 29, 2021 jumla ya wananchi 399 walikuwa wamechanja ndani ya siku tatu.

Maliyao alisema, idadi hiyo ni kubwa tofauti na uchanjaji wa Awamu ya Kwanza, kwani tangu walipoanza zoezi hilo Agosti 5, 2021 hadi Septemba 26, 2021, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ilikuwa imechanja wananchi 1,126, ambapo ilichukua takribani mwezi mmoja na nusu kupata watu hao.

"Zoezi la uchanjaji wa Awamu ya Pili ya chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19 linakwenda vizuri, kwani tangu tumeanza Septemba 27, 2021 tulipata wananchi 111, Septemba 28, 2021 tulipata wananchi 130 na Septemba 29, 2021 tumepata 158 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Hivyo zoezi hili linakwenda vizuri, kwani kwa sasa jumla wananchi 1,525 wamechanjwa tangu Agosti 5, mwaka huu," alisema Maliyao.
Afisa Muuguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Veronica Shehiza akitoa chanjo kwa mwananchi wa Kijiji cha Gare, Kata ya Gare huku Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro (kushoto) akishuhudia zoezi hilo la chanjo ya UVIKO 19. (Picha na Yusuph Mussa).
Afisa Muuguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga Veronica Shehiza akitoa chanjo kwa mwananchi wa Kijiji cha Gare, Kata ya Gare huku Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Kalisti Lazaro (kushoto) akishuhudia zoezi hilo la chanjo ya UVIKO 19. (Picha na Yusuph Mussa).

Maliyao ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, alisema walipewa chanjo 3,450, hivyo ana uhakika zoezi hilo litakwenda vizuri na kumaliza chanjo hizo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news