RC Dkt.Sengati:Mkurugenzi Kishapu ninakupa SIKU SABA ujenzi ukamilike

Na Anthony Ishengoma, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati ametoa siku saba hadi kufikia tarehe 21 mwezi huu kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Bw. Emanuel Jonson kuhakikisha anakamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mwaweja Kata ya Negezi Wilaya ya Kishapu ili wananchi waanze kupata matibabu kijijini hapo.

Dk.Philemon Sengati ametoa agizo hilo baada ya kutembelea ujenzi wa zahanati hiyo na kugundua mapungufu yaliyopo na hivyo kutoa muda wa wiki moja kwa mkurugenzi huyo ili kuwezesha kituo hicho kuanza kutoa huduma kwa kuwa ujenzi huo umechukua muda mrefu bila kukamilika licha ya uwepo wa fedha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati wa kwanza kushoto akiwaongoza baadhi ya wanachi kuelekea Zahanati ya Mwaweja kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo.

Zahanati hiiyoilipaswa kukamilika mwanzoni mwa mwaka huu, baadae ikasimama ambapo ujenzi wake uliendelea tena na ulitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti ili kuwaondolea usumbufu kina mama wajawazito.

Mzee Frank Shija mkazi wa Kijiji cha Mwaweja amesema kuwa, kwa muda mrefu wazee kijijini hapo wamekuwa wakishindwa kupata huduma ya tiba kutokana na kutokuwapo kwa zahanati kijijini hapo na hivyo kupongeza Mkuu wa Mkoa kwa hatua hiyo.

Naye Bi Magreti Kishena akiongea mara baada ya agizo la Mkuu wa Mkoa alisema sasa kuanza kwa huduma katika zahanati hiyo itapunguza adha ya akina mama ambao wamekuwa wakilazimika kukodi mikokoteni kwa lengo lakupata huduma hiyo.

Bi. Mbalu Mkinga ameongeza kuwa wakazi hao wamekuwa wakisafiri kuelekea Kituo cha Afya Ikonda na ili ufike mahala hapo unavuko mto na wakati mwingine mtu anaweza kupoteza Maisha.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Philemon Sengati hayupo pichani wakati wa ukaguzi wa zahanati ya kituo cha Maweja kilichopo Kata ya Negezi Kishapu Shinyanga.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amehitaka Halmashauri ya Kishapu kukamilisha Zahanati ya Maweja ili kituo hicho kisajiliwa na kuingizwa katika orodha ya kupatiwa dawa.

Furaha ya wakazi hao inakuja kufuatia ziara ya Mkuu wa Mkoa kufika kituoni hapo kujionea marekebisho ya ujenzi wa Zahanati hiyo ambapo awali Kamati ya Siasa ya Mkoa ilifika katika zahanati hiyo na kushauri kufanyika marekebisho kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Baada ya kiongozi huyo wa Mkoa kufika katika eneo hilo kufuatilia maagizo ya kamati hiyo aliagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu kuhakikisha nakamilisha mapungufu yaliyopo na ndani wiki moja kazi ya kutoa tiba iwe imeanza.

Post a Comment

0 Comments