BARAZA LA MADAKTARI TANGANYIKA LARIDHIA NA KURUHUSU KUFANYIKA KWA MTIHANI MAALUM KWA WANAFUNZI WA UDAKTARI

NA MWANDISHI MAALUM

Kutokana na kupokea maombi mbalimbali yaliyowasilishwa Baraza la Madaktari Tanganyika limeridhia na kuruhusu kufanyika kwa mtihani maalumu kwa wanafunzi wa Udaktari ambao unatajia kufanyika Disemba 8,2021 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Baraza wa Madaktari Tanganyika, Prof. David Ngassapa ameyasema hayo Oktoba 23, 2021 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kupokea watarajali na kufanya mitihani ya baraza la madaktari kwa waandishi wa habari. Mwenyekiti wa Baraza wa Madaktari Tanganyika Prof. David Ngassapa wakati akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa kupokea watarajali na kufanya mitihani ya baraza la madaktari kwa waandishi wa habari Oktoba 23,2021 jijini Dodoma

“Baraza baada ya kufanya uchunguzi limegundua kuwa wanafunzi hawa wanagawanyika katika makundi matatu kundi la kwanza ni wanafunzi wa mwaka wa mwisho ambao wanakuja kwa ajili ya kufanya mafunzo kwa vitendo ya mwaka wa mwisho wa masomo”amesema

Kundi la pili amesema kuwa ni wanafunzi ambao wamemaliza masomo yao na wanavithibitisho vya kumaliza ambavyo vimethibitishwa na vyuo vikuu vinavyotambulika na tume ya vyuo vikuu.

Ametaja kundi la tatu ni wanafunzi wanaosoma nje ya nchi na wakakumbana na tatizo la kushindwa kurudi vyuoni kwa sababu ya ugonjwa wa UVIKO-19.

“Kundi hili amelielekeza kukamilisha taratibu za kumalizia masomo yao na kufanya mtihani wa mwisho ndipo warudi kujiunga na utarajali”amesisitiza Prof. Ngassapa

Prof. Ngassapa amesema kuwa mtihani huu awali ulilenga wale tu waliokutana na changamoto wakati wa kufanya usajili lakini walikuwa na vigezo vya kufanya mtihani.

”Mtihani huu maalumu ulishapangwa kuwepo na kuna watahiniwa waliokwisha leta maombi ya kurudia mtihani baada ya matokeo,hivyo baraza limeridhia kuwaruhusu nao kufanya kwa marudio ya mtihani huo”amesema Prof. Ngassapa

Aidha amesema kuwa Mtihani huo maalum utafanyika kwa mara hii ya kwanza tu na baraza limeshauri watarajali kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya mtihani.

”Umuhimu wa mitihani hii ya watarajali unalenga kulinda ubora wa taalumu ya Udaktari hasa kutokana na uwepo wa vyuo vikuu vingine viko katika mazingira tofauti hivyo ni vyema wanafunzi na wazazi wote waelewe kuwa baraza linalinda afya zao na wahitimu watakao wahudumia ni lazima wawe na viwango vyenye ubora unahitajika kwa kila Daktari”amesisitiza

Amesema kuwa Baraza la Madaktari Tanganyika ni taasisi iliyopo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news