Dkt.Abbasi:Rais Samia ana jambo na michezo

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa medali mbalimbali jijini Arusha , Oktoba 9, 2021, kwenye kilele cha Michezo ya Riadha Kitaifa.

Dkt.Abbasi amesisitiza kuwa , Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ina jambo na sekta ya michezo.
“Rais Samia ana jambo katika sekta ya michezo, Serikali yake inawekeza sana katika michezo kama sekta ya kimkakati kiuchumi, afya na utalii.

"Ndio maana ameongeza fedha za Timu za Taifa, ametoa asilimia tano ya mapato ya michezo ya kubashiri matokeo kusaidia michezo na mwaka huu tunakwenda kurejesha Taifa Cup ambapo michezo itachezwa kuanzia ngazi ya wilaya na mikoa na kuja kifaifa. Uwekezaji huu umeanza kuleta tija michezoni. Tuwe wamoja tu,”amesema Dkt. Abbasi.
Ametumia fursa hiyo pia kuzitakia kheri na kuzipongeza timu mbalimbali za Tanzania ambazo wiki hii zinacheza/zimetwaa ubingwa wa aina mbalimbali.
Pia ameitakia kheri Taifa Stars inayoshuka uwanjani nchini Benin na ameipongeza Timu ya Taifa ya Kriketi U19 ambayo imeshika nafasi ya tatu Afrika katika mashindano ya Afrika yaliyomalizika nchini Rwanda.

Post a Comment

0 Comments