Dkt.Tulia ashiriki zoezi la kuaga miili sita ya wafanyakazi wa TANESCO waliofariki katika ajali

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ameshiriki zoezi la kuaga miili ya wafanyakazi sita wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO).

Wafanyakazi hao walifariki katika ajali iliyotokea Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Oktoba 22, 2021.
Mheshimiwa Dkt.Tulia ameongoza zoezi hilo leo Oktoba 25,2021 katika Viwanja vya Hospitali ya Igawilo vilivyopo jijini Mbeya.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande kwenye taarifa yake amesema, wafanyakazi hao sita wa TANESCO walifariki kwa ajali ya gari lenye namba za usajili SU 38134.

Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni Physon Maeda (33), Mwamini Kilumile (26), Prisca Mwalongo (26), Silvano Baraka (27), Samuel Lusingu (31) na Salehe Hamis (36).


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news