WAZIRI MAKAMBA AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

NA MWANDISHI MAALUM, UAE

Mhe. January Y. Makamba (Mb), Waziri wa Nishati amewasilisha Ujumbe Maalum wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Mheshimiwa Makamba amewasilisha ujumbe huo maalum kupitia kwa Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, tarehe 24 Oktoba, 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya UAE.

Mheshimiwa Makamba yupo Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Mafuta na Gesi.

Mheshimiwa Makamba katika mazungumzo hayo ameambatana na Mhe. Mohamed Mtonga, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Kamishina wa Mafuta na Gesi, Ndg. Michale Mjinja kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news