Rais Dkt.Mwinyi aainisha faida za ushirikiano wanaoupata kutoka mashirika ya UN

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini sana ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yaliopo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Zlatan Milisic,Mratibu wa UN Zanzibar.Bi.Dorothy Temu Usiri na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui, alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, kuhutubia maadhimisho ya miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN.(Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2021 katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 76 ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa, sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil, Kiwajuni jijini Zanzibar.

Katika maelezo yake, Rais Dkt.Mwinyi alisema kuwa kazi kubwa inafanywa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyopo Zanzibar na imekuwa kiungo muhimu katika kufanikisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Rais Dkt.Mwinyi alisema kuwa, kupitia programu mbalimbali zinazoendeshwa na Mashirika ya UN hapa Zanzibar hasa katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia na hivi sasa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza na inaedelea kunufaika sana na ushirikiano inaoupata kutoka mashirika yote ya Umoja wa Mataifa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Afisa wa WHO .Dr.Vendeun Simon alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho ya Vijana wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa (UN) na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar.Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea mabanda ya maonesho ya Vijana ya kuadhimisha Miaka 76 ya UN, yaliofanyika katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Zlatan Milisic na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar.Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mmoja wa Vijana walioshinda Shindano la Ubunifu Barke Abdullah Ukusi.(hayupo pichani) akielezea Ubunifu wake wa Samaki Mtandaoni, wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Zlatan Milisic na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.

Alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kupata mafanikio katika sekta ya elimu, afya, uhifadhi wa mazingira, kupunguza umasikini na idadi ya vifo vya akina mama na watoto, kuendeleza kilimo, uvuvi na ufugaji, kuwajengea uwezo wafanyakazi, uwezeshaji kiuchumi, kukuza ajira kwa vijana, kuimarisha demokrasia na utawala bora, kudumisha amani na usalama pamoja na maendeleo mengineyo.

Rais Dk. Miwnyi alitumia fursa hiyo kuyakaribisha Mashirika ya UN kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane katika kuendeleza dira ya uchumi wa Buluu, ikiwa ni pamoja na kuendeleeza ushirikiano uliopo katika kuendeleza uvuvi pamoja na wavuvi, kilimo cha mwani na kuliongezea thamani zao hilo.

Hivyo, Rais Dkt.Mwinyi alisema kuwa, mipango ya maendeleo iliyopangwa hapa Zanzibar katika Dira ya Maendeleo ya Zanzibar, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III), na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yote imezingatia mipango mikuu ya mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi alieleza kufurahishwa na kauli mbiu ya Maadhimisho ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu 2021 ambayo ni “Kujijenga upya vizuri zaidi kwa kuweka mifumo bora ya afya” (Building back Better with Health System) na kueleza kwamba kaulimbiu hiyo ina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa dunia sambamba na umuhimu wa pekee kwa maendeleo ya Zanzibar.

Aliongeza kuwa, idadi ya vifo na maambukizi ya maradhi ya UVIKO-19, kwa upande wa Zanzibar haikuwa kubwa kama ilivyotokea katika nchi mbali mbali, lakini athari za kiuchumi ni kubwa zaidi kuliko ilivyotokea katika baadhi ya nchi zilizokuwa na idadi kubwa ya vifo na maambukizi.
Mkurugenzi wa SMIDA Bw. Soud Said Ali akitowa maelezo kuhusiana na Shindano la Kibunifu kwa Vijana Wajasiriamali kuhusiana na Uchumi wa Buluu, wakati wa kuwazawadia washindi wa shindano hilo sambamba na Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Baadhi ya Vijana na Wageni waalikwa katika Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa, wakifuatilia hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Mbunifu Kipimo cha Ujazo wa Mafuta katika Matenki ya Kuhifadhia Mafuta (Computerised System for Oil Measuring) Ndg. Hamid Abdullah Wailu, akitowa maelezo ya ubunifu wake huo wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, yaliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw. Zlatan Milisic akizungumza na kutowa maelezo ya Maadhimisho ya Umoja wa Mataifa kutimiza Miaka 76 tangu kuazishwa kwake, hafla hiyo ya maadhimisho imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Mabalozi Wadogo wanaofanytia Kazi zao Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa, kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mmoja wa Vijana walioshinda Shindano la Ubunifu Barke Abdullah Ukusi.(hayupo pichani) akielezea Ubunifu wake wa Samaki Mtandaoni, wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh.Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Zlatan Milisic.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Husseinn Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 76 ya Umoja wa Mataifa UN, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti na fedha Mshindi wa Shindano la Ubunifu kwa Vijana Wajasiriamali Barke Abdaalah Ukusi kwa Ubunifu wake wa Samaki Mtandaoni na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw. Zlatan Milisic na (kuia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti na fedha Mshindi wa Shindano la Ubunifu kwa Vijana Wajasiriamali Mohammed Wanimo kwa Ubunifu wake wa Mashine ya Kusagia Mwani na (kushoto kwa Rais) Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw. Zlatan Milisic na (kuia kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui.(Picha na Ikulu).

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi sote, tunathamni sana sherehe hizi za maadhimisho kwani zinatupa fursa ya kufahamu na kutafakari historia ya Umoja wa Mataifa, mashirika yake, kazi na majukumu yake pamoja na michango yake kwa maendeleo ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla pamoja na mataifa yote duniani,”alisema Rais Dkt.Mwinyi.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi aliwapongeza vijana wabunifu na kusisitiza haja kwa viongozi wa Serikalini kuwaunga mkono vijana hao ili waweze kufanikiwa zaidi katika ubunifu wao huku akieleza azma ya Serikali ya kuweka eneo maalum kwa ajili ya ubunifu pamoja na kujenga viwanda vidogo vidogo kwa azma ya uchumi wa Zanzibar uweze kuongozwa na teknolojia.

Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui alizipongeza juhudi zinazochukuliwa na UN yakiwemo Mashirika yake katika kuiunga mkono Zanzibar hasa katika sekta ya afya na kueleza jinsi mashirikiano ya pamoja yaliyooneshwa na UN katika kupambana na UVIKO-19 hapa Zanzibar.

Nae Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Zlatan Milisic alieleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na UN kupitia mashirika yake hapa nchini katika kuiunga mkono Tanzania huku akitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania katika kuendeleza uchumi wake hasa kupitia sekta ya Utalii ambapo pia, alitumia fursa hiyo kuahidi na kusisitiza kwamba UN itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuendeleza shughuli zake za maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news