Rais Dkt.Mwinyi atembelea Maonesho Wiki ya Vijana


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Uratibu Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Joakim Mhagama,wakimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kanda Chato, Dkt.Marygoreth Changaluda alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Mazaina Chato.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Ndg. Yussuf Juma akitoa maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Mabaraza ya Vijana Zanzibar, wakati alipotembelea banda lao katika maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja vya Mazaina Chato mkoani Geita. Wananchi wa Chato mkoani Geita wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayuko pichani) akiwahutubia katika viwanja vya Mazaina Chato baada ya kutembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo ikiwa ni shamrashamra za Kilele cha Mbio za Mwenye wa Uhuru na Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Wasanii wa Kikundi cha Taraab cha Wajelajela wakitoa burudani katika viwanja vya Mazaina Chato wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.
WANANCHI wa Chato Mkoani Geita wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika viwanja vya mazaina Chato, baada ya kutembelea Maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia wananchi wa Chato mkoani Geita katika viwanja vya Mazaina, baada ya kutembelea maonesho ya Wiki ya Vijana yaliofanyika katika viwanja hivyo. (Picha zote na IKULU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news