Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi mbalimbali leo Oktoba 8, 2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali katika wizara na taasisi za umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 8, 2021 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni pamoja na;

Kapteni Khatib Khamis Mwadin ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM).

Pia Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Bwana Mudrik Fadhil Abass kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Maji katika Wizara ya Maji, Nishati na Madini.

Uteuzi mwingine ambao Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi ameufanya ni wa Bwana Nassor Shaaban Ameir kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uvuvi Zanzibar (ZAFICO).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyoonwa na DIRAMAKINI Blog, imeeleza kuwa, uteuzi huo unaanzia leo Oktoba 8, 2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwiny. (Picha na Maktaba).

Post a Comment

0 Comments