Rais Samia awasili nchini Scotland kuhudhuria Mkutano wa COP26

NA MWANDISHI MAALUM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 31 Oktoba, 2021 amewasili Glasgow, Scotland kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26).
Mkutano huo unaoshirikisha Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Viongozi wa Kidini, Viongozi wa Taasisi za Biashara, Asasi za Kiraia na watu mashuhuri utafunguliwa rasmi tarehe 1 Novemba, 2021 na kupokea hotuba za viongozi wa Mataifa mbalimbali kuhusu mikakati ya nchi zao katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha, Mkutano huo wa COP26 unakusudia kujadili na kutoa maamuzi ya kuharakisha utekelezaji wa maazimio yaliyopo katika Azimio la Paris katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchis

Mhe. Rais Samia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 2 Novemba, 2021, ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajia kuueleza ulimwengu kupitia hotuba hiyo hatua ambazo Tanzania imepiga katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, changamoto inazokabiliana nazo katika mapambano hayo na pia masuala yanayotakiwa kufanyika ili kupiga hatua katika kufanikiwa kufikia malengo yaliyowekwa.

Mkutano huo umeandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza ambao ndio nchi mwenyeji na Rais wa Mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news