Rais Samia kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi COP 26 nchini Scotland

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuondoka nchini kesho, kwenda Glasgow, Scotland kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP 26).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jackson Msangula,l jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo, Novemba 2, 2021 ambayo itakuwa siku ya pili ya Mkutano huo wa COP 26.

Pia Rais Samia anatarajiwa kukutana na kuzungumza na baadhi Wakuu wa nchi, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja wafanyabiashara wakubwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi hizo na taasisi zao.

"Lengo la Mkutano huo wa COP 26 ni kujadili jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto duniani,"taarifa hiyo imefafanua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news