Waziri Mhagama akemea utoro wa dawa kwa WAVIU

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amekea vitendo vya baadhi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI nchini kukwepa na kusitisha matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo huku wakipatwa na madhara zaidi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza maelezo kutoka kwa Vumilia Constatine kuhusu bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha Faraja cha watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kutoka Kata ya Iduda Wilaya ya Mbeya alipofanya ziara ya kuona shughuli za konga hizo Jijini Mbeya.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua shughuli za watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kutoka katika Konga jijini Mbeya Oktoba 27, 2021, kukagua ujenzi wa Kituo cha Tiba na Matunzo (CTC) Chimala pamoja na ujenzi wa Kituo cha Tiba na Matunzo cha Zahanati ya Igawa Mbarali jijini Mbeya .

Waziri ameeleza kuwa, kumekuwa na kesi za watu kutoroka na kusitisha matumizi ya dawa hizo huku akieleza kuwa ni changamoto inayokwamisha mapambana dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mikeka iliyotengenezwa na umoja wa wanakikundi cha Faraja kinachojumuisha WAVIU kutoka kwenye Konga mbalimbali Wilaya ya Mbeya, anayetoa maelezo ni Bi. Adella Charles.

“Wanaoishi na VVU wote acheni kutoroka dawa bali endeleeni kutumia dawa hizo ili kuendelea kufubaza makali na kuwa afya njema,”amesema Waziri Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za ujasiriamali za WAVIU kutoka katika vikundi mbalimbali walipokutana katika Kata ya Iduda Wilaya ya Mbeya Jijini Mbeya Oktoba 27, 2021.

Amesema, ni wakati sasa jamii kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa dawa hizo kwani zimeendelea kusaidia watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI huku wakiimarika na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji bila kuathiriwa na jambo lolote.

Aidha, amewakumbusha kuendelea kulindana wao kwa wao na kukumbushana matumizi sahihi ya dawa za kufubaza na kupunguza makali ya ugonjwa huo huku akiwasii kuendelea kujiandikisha na Bima ya Afya ili kusaidia kupata huduma za afya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa sweta lililofumwa na wanakikundi cha WAVIU kutoka katika Konga za watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI alipotembelea kukagua shughuli za ujasiriamali wanazoendelea nazo katika Wilaya ya Mbeya, anayetoa maelezo ni Bi. Adella Charles.

“Hakikisheni kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake kwa kusisitiza matumizi sahihi ya dawa bila kukwepa na endeleeni kuhakikisha kila anayeishi na VVU anakuwa na Bima ya Afya, kwani itarahisisha kupata huduma za afya, mkakati huu ni mzuri napongeza sana,”amesema.

Aidha alitumia fursa hivyo kuendelea kuwasihi wanaume kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kwani imeonekana ni kundi ambalo lipo nyuma katika kujitokeza kujua hali zao.

Aidha, aliagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuendelea kuunga mkono mapambano hayo huku akimtaka kutoa kipaumbele kwa WAVIU katika utoaji wa mikopo isiyo na riba ili kuwakwamua na changamoto za mitaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabishiwa zawadi ya picha aliyochorwa na Mmoja wa wajasiriamali kutoka katika Konga za watu wanaoishi na VVU Bw. Faraja alipotembelea kuona shughuli za uzalishaji kujiongeza kipato. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bi. Leticia Mourice.

“Halmashauri endeleni kuchangia jitihada za watu wanaoishi na VVU na hakikisheni mnakuwa na kanzi data itayosaidia kuwafahamu na kuwafikia kwa wakati hii itasaidia katika shughuli za kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao,”alieleza Waziri.
Akitoa taarifa ya hali ya masuala ya UKIMWI, Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Mbeya,Douglas Kisunga alisema, halmashauri ina jumla ya konga kata 32 na vikundi wezeshi 54 vya shughuli za mwitikio wa masuala ya UKIMWI na kuhamasisha upimaji na kuwaunganisha WAVIU kutambuana na kusaidiana katika kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Dkt. Leonard Maboko wakiangalia zawadi picha maalum iliyoichorwa na mmoja wa wajasiliamali kutoka kikundi cha watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Bw. Faraja wakati wa ziara yake Mkoani Mbeya kukagua shughuli zao.

Aliishukuru Serikali kuendelea kuwatambua na kuwaunga mkono katika shughuli zao za kila siku huku akieleza mafanikio ya konga hiyo, kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji wamefanikiwa kuwa na umoja wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, na kupata huduma za tiba na matunzo na kuhamasisha watu kujitokeza zaidi.

“Mwanzo WAVIU waliojitokeza kwa uchache ambapo walikuwa 53 tu, hadi sasa wamejitokeza na kufikia 1129 na wapo huru, wanaishi kwa raha na wanafuata maelekezo ya Serikali huku wakifurahia maisha,”amesema Kisunga.

Aidha, alieleza kwa kipindi cha Juni hadi Julai konga imefanikiwa kurudisha watoro wa dawa 132 ambapo wanaume ni 58 na wanawake 74 na kuhakikisha wanabaki katika huduma za tiba na matunzo.

Alifafanua kuwa, Konga zimefanikiwa kuwa mstari wa mbela katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, kuendelea kuhamasisha upimaji wa hiari na matumizi ya dawa kwa kujilinda na kulinda wengine na kumekuwa na uwazi wa watu kujitokeza kueleza hali zao.

“Katika kujitokeza kupima na kujua hali wanaume wamekuwa na mwitikio mdogo ambapo kwetu waliojitokeza ni 622 wanaume na wanawake 1407 hivyo kundi la wanaume bado lipo chini tuendelee kuwahamasisha kujitokeza kujua hali zao ili wakikutwa na maambukizi wajiunge katika huduma za tiba na matunzo,”alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akieleza mikakati ya kuendelea kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI wakati wa ziara hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini, Dkt. Leonard Maboko alitoa rai kwa kila mtanzania kutambua kuwa ugonjwa huu upo, watu wajitokeze kupima na kujua hali zao ili kuendeleza mapambano hayo na kupunguza hali ya maambukizi mapya nchini.
Baadhi ya Washiriki kutoka katika Konga za Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Wilaya ya Mbeya wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani).(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news