NA LSUNGU HELELA-WMU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) Prof.Romanus Ishengoma ( katikati) ambapo Bodi hiyo imeongezewa muda wa kuendelea kutekeleza majukumu yake kisheria hadi pale itakapotangazwa Bodi mpya katika makabidhiano yaliyofanyika leo Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taff, Lulu Ng’wanakilala. Ametoa uamuzi huo mapema leo Jijini Dodoma kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akikabidhiwa taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Wenyeviti wa Bodi za Wakurugenzi wa Bodi hizo wakiwa wameambatana na Wajumbe wao.
Dkt.Ndumbaro amewaeleza Wajumbe wa Bodi hizo kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kisheria katika Taasisi hizo hadi pale atakapotangaza Bodi mpya huku akitaja moja ya sababu iliyomfanya kuchukua uamuzi kuwa ni kuridhishwa na utendaji kazi wa Bodi zote mbili.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akikabidhiwa taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wantamapori Tanzania ( TAWA) Meja Jenerali Hamisi Semfuko ( kulia) ambapo Bodi hiyo imeongezewa muda wa kuendelea kutekeleza majukumu yake kisheria hadi pale itakapotangazwa Bodi mpya katika makabidhiano yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.”Ninaweza nikatangaza Bodi mpya hata kesho au nisitangaze Bodi hizo kwa kipindi cha miaka mitatu ninachosisitiza kipindi chenu kitaisha pale tu nitakapotangaza Bodi mpya,”amesisitiza Dkt.Ndumbaro.
Katika hatua nyingine, Dkt.Ndumbaro ameitaka Bodi ya TAWA kuhakikisha inaisimamia taasisi hiyo ipasavyo kwa kuhakikisha inaendeshwa kibiashara na sio kama ilivyo sasa ambapo utendaji kazi wake wa kushughulikia changamoto za Wawekezaji umekuwa ni wa taratibu sana hali inayowakazwa Wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika maeneo wanayoyasimamia.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) ambapo amewataka kuhakikisha uzalishaji wa asali unaongezeka kutokana na uhitaji mkubwa wa soko la ndani na nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) mara baada ta kumaliza kikao kilichofanyika leo Jijni Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Meja Jenerali ( Mst) Hamisi Semfuko
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa kwenye picha na pamoja na Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) Prof.Romanus Ishengoma ( katikati) ambapo Bodi hiyo imeongezewa muda wa kuendelea kutekeleza majukumu yake kisheria hadi pale itakapotangazwa Bodi mpya katika makabidhiano yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) mara baada ya kumalizika kikao cha kukabidhi taarifa ya utendaji wa kipindi cha miaka mitatu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania ( Taff) Prof.Romanus Ishengoma ( wa pili kulia)
Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akizungumza kabla ya kukaribishwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali (Mst.) Hamis Semfuko kwa ajili ya kukabidhi taarifa ya Utendaji ya miaka mitatu ya Bodi hiyo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( wa kwanza kushoto) katika,kikao hicho kilichofanyika leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( kulia) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Misitu Tanzania (Taff) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Godwin Gondwe mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bodi ya Taff kilichofanyika leo Jijini Dodoma ambapo Waziri Ndumbaro ameiongezea Bodi hiyo muda wa kuendelea kufanya kazi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ( kulia) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Misitu Tanzania (Taff) ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Misitu Tanzania Dkt. Tully Msuya mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bodi ya Taff kilichofanyika leo Jijini Dodoma ambapo Waziri Ndumbaro ameiongezea Bodi hiyo muda wa kuendelea kufanya kazi. ( PICHA NA LUSUNGU HELELA- MALIASILI NA UTALII).”Nataka mkafanye kazi yule atakayetaka kutoboa mtumbwi tukimbaini tutamvisha mawe na kumtosa majini ili atuache sisi tuendelee na safari yetu,” amesisitiza Dkt.Ndumbaro.
Kwa upande wao Wenyeviti wa Bodi hao Meja Jenerali (Mst.) Hamisi Semfuko wa TAWA pamoja Prof. Romanus Ishengoma wa Taff wamemshuku Waziri Ndumbaro kwa imani kubwa aliyoionesha kwao na kuahidi kuwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa maslahi mapana ya taasisi hizo na kwa niaba ya Watanzania wote.