Dean Smith ni kocha wa tano EPL kubebeshwa virago msimu huu

NA GODFREY NNKO

Uongozi wa Klabu ya Aston Villa umekiri wazi kuwa, katika msimu huu hawajaona maendeleo yoyote ya timu yao, hivyo wamelazimika kuchukua maamuzi magumu.

Maamuzi hayo yameenda sambamba na kumfuta kazi kocha Dean Smith mwenye umri wa miaka 50 ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu.
Dean Smith anaungana na wenzake kuwa wa tano kuondoka msimu huu katika klabu tofauti tofauti EPL.

Makocha wengine ambao walipoteza ajira zao ni Xisco Munoz wa Watford,Steve Bruce wa Newcastle United, Nuno Espirito Santo wa Tottenham na Daniel Farke wa Norwich City.

Dean anaondoka baada ya Ijumaa iliyopita kukiongoza kikosi cha Villa kukutana na kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton katika dimba la St Mary's.

Aliyevuruga mipango yote katika mchezo huo wa tano mfululizo kupoteza msimu huu ni Adam Armstrong ambaye aliwapa ushindi waajiri wake Southampton ndani ya dakika za mwanzo za mchezo huo kipindi cha kwanza.

Matokeo ambayo yalimlazimisha Mkurugenzi wa Aston Villa, Christian Purslow kudai wazi kuwa “Msimu huu hatujaona maendeleo katika kikosi chetu, kiwango na nafasi tuliyopo hailingani na malengo yetu, tumeamua kufanya mabadiliko mapema kumpa nafasi kocha mpya kuja na kuonyesha maendeleo katika kikosi chetu,”amesema.

Dean Smith alitajwa kuwa kocha wa Villa Oktoba 2018 ambapo alikiongoza kikosi hicho kupanda daraja katika msimu wake wa kwanza, lakini kwa sasa imeonekana mambo hayapo sawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news