Feisal Salum ndiye mchezaji bora Oktoba, kocha bora ni Nasreddine Nabi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Feisal Salum ambaye ni kiungo wa Yanga SC ameteuliwa kuwa, Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku kocha wake ambaye ni raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi akiteuliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 8, 2021 na Bodi ya Ligi, mshambuliaji wa Polisi Tanzania, Vitalis Mayanga ameteuliwa Mchezaji Bora wa mwezi wa kwanza wa msimu, Septemba huku kocha wake, Malale Hamsini akiteuliwa Kocha Bora mwezi huo wa tisa.

Aidha, Tumaini Ikomba ameteuliwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja mwezi Septemba kwa nzuri Uwanja wa Black Rhino uliopo Karatu mkoani Arusha na Modestus Mwaluka amekuwa Meneja Bora wa Oktoba kwa kazi yake nzuri Uwanja wa Sokoine uliopo jijini Mbeya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news