Hakuna mgao wa umeme nchini-TANESCO

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limesema kuwa, kwa sasa hapa nchini hakuna mgao wa umeme.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande wakati wa mahojiano katika kipindi cha Joto la Asubuhi kinachorushwa na EFM ya jijini Dar es Salaam.

Hakuna tatizo la mgao wa umeme, ili kuwe na mgao wa umeme ina maana umeme unaozalishwa unakuwa haukidhi mahitaji.

Kwa sasa tunazalisha MW 1,600 na matumizi ya kiwango cha juu ya umeme kilichorekodiwa wiki iliyopita ni MW 1,273.42.

Katika kuleta umeme kwa wateja wetu kuna mambo matatu, kwanza ni kuzalisha umeme.

Pili ni usafirishaji umeme na tatu ni usambazaji. Matatizo mengi ya kukatika umeme yanatokana na eneo la usambazaji.

Idadi ya wateja imeongezeka zaidi kutaka kuunganishiwa umeme, na katika robo ya kwanza tumewaunganisha wateja 150,000 kutoka kwenye lengo la kuwaunganisha wateja 75,000.

Sisi ni shirika la huduma, kazi yetu ni kutoa huduma kwa wateja, tuna kazi kubwa ya kutoa huduma kwa wateja. Hatuhitaji ile uwe na rafiki unayemjua ndipo upate huduma kwa haraka, na kwenye tumeongeza ufanisi kwa kuwa na matumizi ya mifumo zaidi kuliko mikono.

Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa, hiyo kwake ni heshima kubwa ya kuaminiwa katika kulitumikia Taifa kupitia shirika hilo.

Hakuna heshima kubwa kama kupata nafasi ya kulitumikia Taifa lako. Thamani yake ni kubwa sana katika hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news