Mhandisi Kasekenya aridhishwa na kasi ujenzi wa Daraja la Msingi

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa Daraja la Msingi lililoko wilayani Mkalama mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mhandisi Gofrey Kasekenya akikagua namna ujenzi wa daraja la Msingi wilayani Mkalama mkoani Singida unavyoendelea.

Daraja hilo ni miongoni mwa madaraja makubwa yaliopangwa kujengwa tangu wakati wa uhuru hivyo kukamilika kwake kutaleta chachu ya maendeleo kwa wakazi wa mikoa ya Singida, Simiyu na Manyara.
Muonekano wa daraja la Msingi lenye urefu wa mita 100 na upana wa mita 10 ambalo ujenzi wake unaendelea wilayani Mkalama mkoani Singida.

“Tunapoadhimisha miaka sitini ya uhuru wa Tanzania Bara ni fahari kubwa kuona daraja hili ambalo ujenzi wake ulikuwa ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere sasa umefikia asilimia 75 kukamilika,”amebainisha Naibu Waziri Kasekenya.
Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Kyong Dong, Mhandisi Mazige Seif anayesimamia ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi kilomita 50.3 akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Gofrey Kasekenya (kushoto), alipokagua ujenzi huo (katikati), ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi John Mkumbo akifuatilia.

Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Singida, Mjadisi Joseph Masige amesema daraja hilo lenye urefu wa mita 100 na upana wa mita 10 pamoja na barabara za maingilio zenye urefu wa KM 1 linajengwa na mkandarasi mzawa GEMEN ENGINEERING CO. LTD kwa gharama ya shilingi bilioni 10.9 na linatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwakani.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida, Mhandisi Joseph Masige akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Gofrey Kasekenya alipokagua daraja la Sibiti (kushoto), ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Simiyu, Mhandisi John Mkumbo akifuatilia.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Kasekenya amekagua daraja la Sibiti lenye urefu wa mita 82, ambalo ujenzi wake umekamilika na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kulinda miundonmbinu ya daraja hilo ili lidimu kwa muda mrefu.

Amewataka Meneja wa TANROADS mkoa wa Simiyu, Mhandisi John Mkumbo na wa Singida, Mhandisi Joseph Masige kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda madaraja na kuhakikisha kingo za daraja hilo zinaimarishwa ili kuliwezesha kukabiliana na changamoto za mafuriko wakati wa mvua kubwa.

Daraja la Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida kupitia wilaya za Meatu na Mkalama linaunganisha kwa njia fupi mikoa ya Kaskazini na Kanda ya Ziwa na hivyo litachochea unafuu wa huduma za kijamii na biashara baina ya wakazi wa mikoa hiyo.
Muonekano wa daraja la Sibiti linalounganisha mikoa ya Simiyu na Singida kupitia wilaya za Meatu na Mkalama ambalo ujenzi wake umekamilika.
Muonekano wa barabara ya Maswa-Mwigumbi kilomita 50.3 ambayo ujenzi wake kwenye maeneo korofi unaendelea.(PICHA ZOTE NA WUU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news