Msanii Davido atoa fedha Bilioni 1.4/- alizochangiwa kwa ajili ya 'Birthday' kusaidia watoto yatima

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

DAVIDO Adedeji Adeleke maarufu kama Davido ambaye ni mwimbaji nyota, mwandishi wa nyimbo na produza kutoka nchini Nigeria ametoa Shilingi Bilioni 1.4 kwa ajili ya kwenda kwenye vituo vyote vya watoto yatima nchini Nigeria.
Nyota huyo wa muziki ametoa taarifa hiyo katika ukurasa wake wa Twitter ambapo ameeleza kuwa kiasi chote alichochangiwa kwa ajili ya siku yake ya kuzaliwa ameamua kukitoa kwa watoto hao.

Davido amesema kuwa, anamini, ''Tunainuka kwa kuinua wengine''

Ni baada ya kuchangiwa kiasi cha Naira Milioni 200 na yeye ameamua kutoa kiasi cha Naira milioni 50 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 250 huku jumla Kuu ikiwa ni Shilingi Bilioni 1.4.

Post a Comment

0 Comments