Mtoto wa Kizungu Briana ampa jeuri Harmonize, awakataa marafiki Instagram

NA GODFREY NNKO

RAJAB Abdul Kahali (Harmonize, Konde Boy au Teacher, Tembo na mengine mengi) ambaye ni miongoni mwa waimbaji staa na mtunzi wa muziki, mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania baada ya siku moja kutangaza yupo katika uhusiano mpya na mrembo anayejulikana kwa jina la Briana kutoka nchini Australia, amewapa kisogo marafiki zake Instagram na kubaki na Briana wake.
Uhusiano huo umeingia katika ukurasa mpya, baada ya kudhirisha kuwa, yeye Harmonize bila Briana hakuna chochote kinachoendelea hapa Duniani.

Licha ya kuwa na watu ambao anawasimamia kupitia Lebo yake ya Konde Music Worldwide na wanaomsimamia, msanii huyo mwenye wafuasi milioni 7.6 katika ukurasa wa Instagram, Novemba 17, 2021 ameamua kujiondoa (un-follow) kwa watu wote aliokuwa amewafuata katika ukurasa wake wa Instagram kisha akajumuika na mpenzi wake pekee, Briana.

Uhusiano huo ni mwendelezo wa Harmonize kuwa moto pindi anapozama katika ulimwengu wa mahaba rejea kwa Jackline Wolper, Sarah wa Italia na Kajala Masanja.

Kwani mara nyingi humuweka wazi mwanamke wake katika mitandao ya kijamii na kuwaacha hoi mashabiki zake na hata wanapoachana huwa anaachia ujumbe mrefu na wakati mwingine kumtungia wimbo.
Mmoja wa wachambuzi wa masuala ya Kidigitali ameieleza DIRAMAKINI Blog kuwa, uamuzi wa watu maarufu kama Harmonize kujichukulia maamuzi ya haraka haraka hususani kujiondoa kwa marafiki na wadau wa karibu mitandaoni inaonyesha udhaifu mkubwa sana.

"Hatua hii kisanaa na hata kibiashara ambapo wengi wetu tunatumia hii Mitandao ya kijamii kuwasiliana na watu wetu wa karibu na hata kutangaza biashara zetu si njema. Kwa Harmonize huu ni udhaifu mkubwa, maana mashabiki Milioni 7 wanaokufuafilia,unakuwa unabandika andiko lako tu, hauwajibu jumbe zao, lakini pia inafikia hatua unakataa wote unajiona wewe na mpenzi wako ndiyo wa maana, hii ni changamoto sana, wajisahihishe na kujitathimini imani ya mashabiki wao na kuwakubali ndiyo inayowapa shibe na kiburi, hivyo thamani kwao ni jambo muhimu sana,"ameeleza Mtalaamu huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news