Profesa Jeckoniah ataja mambo ambayo yakifanyiwa kazi yanakwenda kuzika tofauti za kijinsia katika kuhifadhi misitu ya asili nchini

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAJUMUISHO 12 na Mapendekezo nane yakifanyiwa kazi tofauti za kijinsia katika shughuli za uhifadhi wa misitu ya asili katika uvunaji na utumiaji wa rasilimali zinazopatikana katika misitu ya asili yataleta tija.
Mtafiti na Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa John Jeckoniah akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa usimamizi Shirikishi wa Misitu Mkoa wa Morogoro na Lindi.

Mtafiti na Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa John Jeckoniah ameyasema hayo Novemba 17,2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa usimamizi Shirikishi wa Misitu Mkoa wa Morogoro na Lindi.

Alisema mapendekezo hayo yalijiri baada ya kufanya utafiti ili kujua mgawanyo wa majukumu katika shughuli za uhifadhi wa misitu ya asili na ushiriki wa makundi mbalimbali ya kijinsia kufikia rasilimali zitokanazo na misitu ya asili.

“Lengo lingine la utafiti huo tulioufanya katika Wilaya ya Kilosa, Mvomero na Morogoro Vijijini ulilenga kuibua masuala gani ya muhimu ya kijinsia ambayo yapo kwenye shughuli nzima za uhifadhi wa misitu ya asili inayosimamiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC), ” alisema Jockeniah.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) Bettie Luwuge akizungumza katika mkutano.Wananchi wa Kijiji cha Ndole wakiwa kwenye mkutano huo.Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ndole Ezekiel Isaya akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinda Ezekiel Mhando.Waandishi wa habari wakichukua taarifa mbalimbali katika mkutano uliofanyika Kijiji cha Ndole wilayani Mvomero.Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi akizungumza kwenye mkutano huo.

Alitaja lengo lingine kuwa ni kutaka kuangalia kuna uelewa gani kuhusu kutumia rasilimali mbalimbali zilizopo kwenye misitu ya asili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo baadhi ya wajumbe wa kamati za maliasili wa Kijiji cha Ndole kilichopo Kata ya Kinda wilayani Mvomero mkoani hapa na Wajumbe wa Kijiji cha Ihombwe wilayani Kilosa walilishukuru shirika la TFCG kwa kuwapatia mafunzo ya uhifadhi wa Misitu.

Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ndole Ezekiel Isaya alisemia baada ya kupata elimu hiyo Jamii imekuwa na uelewa mpana wa uhifadhi misitu na matumizi bora ya ardhi.Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndole Adriano Paul akizungumza kwenye mkutano huo.Mwenyekiti wa Kamati ya Jamii wa kijiji hicho Mathias Chambo akizungumza kwenye mkutano huo.Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili wa kijiji hicho Anna Mohamed akizungumza kwenye mkutano huo.Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinda, Fortunata George akichangia jambo kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Jamii wa kijiji hicho Mathias Chambo alisema licha ya kupanga matumizi bora ya ardhi na mpango wa mkaa endelevu changamoto kubwa ni soko la kuuza bidhaa hiyo baada ya wafanyabiashara kuacha kwenda kuinunua.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili wa kijiji hicho Anna Mohamed alisema baada ya kupata elimu hiyo hivi sasa wanawake wamekuwa wakishiriki katika biashara ya mazao ya misitu kama wanavyofanya wanaume hivyo kutekeleza dhana nzima ya kuzingatia jinsia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news