Rais Dkt.Mwinyi ajumuika na wananchi katika maziko ya Baba mzazi wa mjane wa Maalim Seif


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume, na kulia kwa Rais ni mtoto wa marehemu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa sala ya Jeneza kuusalia mwili wa Baba Mzazi wa Mjane wa Maalim Seif Sharif Hamad, Mama Awena Sanani Masoud iliofanyika katika Msikiti wa Masingini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja leo Novemba 22,2021 na kushoto kwa Rais ni Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi. (Picha zote na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwafariji watoto wa marehemu Sanani Masoud, baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza iliofanyika katika Msikiti wa Masingini Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutoa mkono wa pole kwa Mjane wa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, Mama Awena Sanani na familia yake, alipofika nyumbani kwa marehemu Masingini Wilaya ya Magharibi”A” Unguja kutoa mkono wa pole kwa familia.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea Baba Mzazi wa Mjane wa Maalim Seif Sharif Hamad, Mama Awena Sanani Masoud, alipofika nyumbani kwa marehemu kutoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu.

Post a Comment

0 Comments