Rais Dkt.Mwinyi atoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kwa kula samaki wa kasa anayesadikiwa kuwa na sumu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia za marehemu waliofariki kufuatia kula samaki wa kasa anayesadikiwa kuwa na sumu huko katika Kijiji cha Msuka Taponi, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuziomba familia za marehemu hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu awalaze Marehemu wote mahala pema peponi, Amin.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu kuwaponya kwa haraka waliodhurika baada ya kula samaki huyo anayesadikiwa kuwa na sumu.

Rais Dkt. Mwinyi katika salamu zake hizo za pole amesema kwamba, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara yake husika itaendelea kuhakikisha wale wote waliodhurika wanaendelea kupatiwa tiba sahihi ili waweze kurudi katika hali nzuri za kiafya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news