Simba SC yatembeza kichapo cha mabao 3-0 kwa Red Arrows

NA GODFREY NNKO

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wametembeza kichapo cha 3-0 kwa Red Arrows FC ya nchini Zambia.
Ni katika mtanange ambao umepigwa leo Novemba 28,2021 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Aidha,licha ya dimba kujaa maji, Simba SC imecheza kandanda safi na kufanikiwa kuondoka mapumziko wakiwa na faida ya mabao mawili yaliyofungwa na Benard Morrison pamoja na Meddie Kagere.

Kipindi cha pili kilianza Simba SC ikionekana bado inahitaji magoli zaidi licha jya kuwa mbele kwa mabao mawili ambapo dakika 79 ilifanikiwa kupata bao la tatu kupitia tena kwa nyota wao Benard Morrison.

Kwa matokeo hayo,Simba inahitaji ushindi wowote ama sare katika mchezo ujao ili waweze kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho ambapo Red Arrows watakuwaa nyumbani kwenye mchezo huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news