Rais Dkt.Mwinyi: Tumedhamiria kuinuia uchumi wetu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali inatumia nguvu zote kuongeza fedha kwenye sekta za kiuchumi, hivyo amewataka watendaji wote watakaokabidhiwa dhamana ya kusimamia fedha hizo kuwa wakweli na waaminifu ili ziweze kuwafikia wananchi wote waliolengwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Saba.Alhaj Dkt.Ali Mohamed Shein, alipofika nyumbani kwake Kibele Wilaya ya Kati Unguja kumpa mkono wa pole kwa kufiwa na kaka yake.(Picha na Ikulu).

Alhaj Dkt. Mwinyi amesema hayo katika salamu zake kwa waumini wa Dini ya Kiislamu waliojumuika pamoja katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika Masjid Arafaa, Mombasa jijini hapa.

Amesema, kudorora kwa uchumi wa Zanzibar kulikotokana na ugonjwa wa Uviko 19, kumeifanya Serikali kuchukua kila hatua ikiwemo kutafuta mikopo ili kupata fedha kwa lengo la kupunguza makali ya ugumu wa maisha yanayowakabili wananchi, baada ya kuathirika kwa sekta mbali mbali, hususan sekta ya Utalii.

Amesema, Zanzibar imejaliwa kuwa na neema ya kuwa na amani , umoja na mshikamano, hivyo kuna haja ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa msingi kuwa mambo hayo ndio msingi wa maendeleo.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Arafa Mombasa Wilaya ya Magharibi “B”Unguja leo 19-11-2021.(Picha na Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Masjid Arafa Mombasa Wilaya ya Magharibi “B”Unguja, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid hiyo leo 19-11-2021.(Picha na Ikulu).

Amesema, kila mmoja sehemu alipo,hususan kwa watendaji wa taasisi zinazotoa huduma kufahamu jukumu alilonalola kuhakikisha anakuwa mkweli na muaminifu

“Kila mmoja sehemu alipo awajibike na kumuomba Mwenyezi Mungu li tuweze kufanikiwa,"amesema.

Mapema, Katibu wa Mufiti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume, aliwaomba waumini hao kumuombea dua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Mwinyi ili aweze kutekeleza malengo yake na kubainisha neema kubwa iliobarikiwa Zanzibar kwa kuwa na kiongozi mkweli, muaminifu na mwenye kusononeshwa na shida za wananchi wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Salum Maridhia (hayupo pichani) akisoma dua baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Arafa Mombasa Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.(Picha na Ikulu).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mwanasiasa Mkongwe Zanzibar Bi Tereza Olbam Ali, alipofika nyumbani kwake miembeni kumtembelea na kumjulia hali yake.(Picha na Ikulu).

Nae, Khatibu katika Sala hiyo ya Ijumaa Sheikh Ali Yunus, aliwataka waumini wanaopewa dhamana katika taasisi zinazototoa huduma kuwa wakweli na waaminifu, kama kigezo cha kumfuata Mtume Muhammad (SAW).

Aliwakumbusha waumini hao wajibu wa kupendana, kuoneana huruma pamoja na kufanyiana wepesi katika maisha.

Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar Alhaj Dk. Mwinyi ,alipata nafasi ya kufika nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu saba Alhaj Dk. Ali Mohammed Shein, na kutoa mkono wa pole kutokana na kifo cha kaka yake Shein Mohamed Shein, aliefariki dunia mapema wiki hii.

Aidha, Alhaj Mwinyi alifika nyumbani kwa Mwanasiasa mkongwe hapa nchini, Thereza Alban Ali na kumpa mkono wa pole kutokana na kifo cha mtoto wake kilichotokea hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments