Simba SC yatoa dozi kali kwa Ruvu Shooting

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SIMBA SC imetoa dozi kwa Ruvu Shooting ya mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wa Mnyarwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere mawili dakika ya 18 na 37.

Sambamba na Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis dakika ya 44, wakati la Ruvu limefungwa na Elias Maguli dakika ya 70.

Simba inafikisha alama 14 baada ya mechi sita na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja na watani, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Ruvu inabaki na alama sita za mechi sita ikishukia nafasi ya 11.

Wakati huo huo, mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Benedictor Jaboc dakika ya 46 limewapa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Coastal inafikisha alama saba baada ya mechi sita na kusogea nafasi ya 10, wakati Polisi Tanzania inabaki na alama zake 10 za mechi sita katika nafasi ya tatu.

Aidha, Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Mbeya Kwanza Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mjini Rukwa.

Kwa matokeo hayo, Prisons inahama mkiani hadi nafasi ya 12 baada ya ushindi wa leo katika mchezo wa sita.

Aidha,Mbeya Kwanza inabaki na alama zake saba za mechi sita, ikishukia nafasi ya saba kutoka ya sita katika Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Post a Comment

0 Comments