Serikali yatoa wito kwa maafisa maendeleo ya ustawi wa jamii Pwani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAAFISA Maendeleo na Ustawi wa Jamii mkoani Pwani wametakiwa kubadilisha mitazamo na fikra za wananchi wa mkoa huo ili waondokane na vitendo vya unayanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na maofisa hao ambapo alisema elimu tu ndiyo itakayosababisha kukabilina na changamoto hizo.

Jingu amesema kuwa, suala la ukatili ndani ya jamii ni changamoto kubwa na ni la kidunia, lakini kitakachosaidia ni wao kutoa elimu na kubadilisha mawazo na mitazamo ya wananchi ili waweze kujua kufanya hivyo ni kosa la kusababisha kuendelea kwa umaskini

“Baadhi ya vitendo vya ukatili kwenye jamii ni pamoja na watoto kubakwa, kutopelekwa shule, wanaozeshwa pia unyanyasaji wa wanawake au kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na haya yanaendana na umaskini matatizo haya yanahitajika mabadiliko ya fikra mitazamo nyie ndiyo kazi yenu kubadilisha jamii kwani nyie ni wahandisi wa jamii,”amesema Dkt. Jingu.
 
Amesema, lazima watu wajiulize kwanini kunakuwa na wimbi la watoto wanaokinzana na sheria ambapo inaonyesha kuwa watendaji hao wajatimiza wajibu wao hawajiulizi kwa nini watoto hawaendi shule wanajihusisha na wizi na uuzaji wa bidhaa ambapo Sheria ya Mtoto kifungu 94 inasema kuwa serikali za mitaa na vijiji wajibu wa kulinda usatwi wa watoto sehemu walipo kwa kuorodhesha watoto walio kwenye mazingira hatarishi na kuhakikisha ofisa ustawi wa jamii asaidine na mamlaka ya serikali ya mtaa eneo husika kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa.
“Ofisa maendeleo ya jamii kazi yenu ni kubadilisha fikra za watu, kwani mmeshindwa kubadili fikra za wafugaji kubadilisha fikra za wazazi hao ili waachane na vitendo vya kutowalinda watoto kwa kuwaozesha wakiwa bado wadogo kwa sasa mazingira yamebadilika lazima twende na wakati mkoa wa Pwani siyo maskini bali Pwani ni tajiri sana kwa ardhi, kwani ina rutuba ukiuliza watu wanaotoka mkoa wa Pwani wanauza bidhaa Kariakoo wengi hawatoki Pwani wanatoka mikoa mingine hivyo mkiwabadilisha fikra hali hii itaondoka,”amesema Dkt.Jingu.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Mhandisi Mwanasha Tumbo amesema kuwa, kada hizo ni muhimu wanafanya kazi kubwa licha ya changamoto walizonazo kwani hawana magari wanatekeleza majukumu yao ya msingi wanatekeleza licha ya kuwa mapungufu ya kutoismamia vizuri sheria ya mtoto kwani kuna watoto wengi wanafuga wanatembea na ng’ombe na wao bado hawajaliona kwani watoto anatumikishwa wanapaswa kuwasimamia.
Mhandisi Mwanasha amesema kuwa, maofisa hao wanapaswa kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi na kuwachukulia hatua wazazi wanaoishindwa kuwapeleka watoto shule na walikubaliana kufanya kazi kama timu moja lazima watu wanapofanya miradi washirikishane ili kuondoa tofauti na watachukua hatua kwa watakaoshindwa kuwashirikisha.

Amesema kuwa, maendeleo ya jamii ni masuala mtambuka kila eneo tutasimamia watu wafanyakazi kwa pamoja na kabla ya mwaka huu watafanya msawazo wa watumishi na kama kuna mapungufu tutawajulisha hadi Januari mwakani kila mtu atajua yuko wapi.

Naye Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka wizara hiyo, Hanifa Selengu amesema kuwa na ushirikiano na wizara ya Tamisemi itaaidia kuondoa tatizo la uratibu kwa wataalamu wa maendeleo ya jamii kazi ya maendeleo ya jamii ni kuhakikisha inashsirikisha wananchi kwenye shughuli za maendeleo na wakifanya vizuri taifa litaweza kujitegemea.

Selengu alisema kuwa, idara itoe maoni ya kitaalamu kwa uongozi kwenye miradi kwani wao ni watu wa kwanza kuwaandaa wananchi katika suala la maendeleo ya jamii na wakiandaliwa vizuri watashiriki vyema mauala ya maendeleo kuanzia ngazi ya jamii ili wajiletee maendeleo.

Naye Kamishina wa Ustawi wa Jamii, Dk. Nandera Mhando alisema kuwa, wapo tayari kuwezesha watendaji kuondokana na changamoto ambao wako kwenye mchakato wa kutafuta usafiri na watazifanyia kazi na kuangalia namna ya kushirikiana.

Awali akisoma taarifa ya mkoa ofisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Pwani, Asha Itewele alisema kuwa kwenye madawati ya ustawi wa jamii jumla ya mashauri kwa mwaka 2020/2021 mashauri 4,035 yalipokelewa kwenye Halmashauri kati ya hayo migogoro ya ndoa 724 iliyoripotiwa sawa na asilimia 17.9, matunzo watoto 2,129 sawa na asilimia 52.7 watoto nje ya ndoa ni 1,182 sawa na asilimia 29.2 mahakama 12 hukumu 90.

Itewele alisema mashauri yalikuwa 2,851,ya kingono yalikuwa 2,512 kimwili yalikuwa 285 kiuchumi 577, kutekelezwa 565, mahakamani 252, yaliyohukumiwa 94 mashauri ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto 3,795 yalipokelewa na kupatiwa huduma kwenye kituo cha huduma cha one stop centre kilichopo Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.

Post a Comment

0 Comments