Tanzania yatembeza kichapo cha 2-1 kwa Morocco michuano ya CANAF

NA JOHN MAPEPELE,WUSM

TIMU ya Tanzania ya soka kwa wanaume kwa wenye ulemavu Tembo Warriors imeanza vizuri mashindano ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu barani Afrika (CANAF 2021) baada ya kuibamiza vibaya mabao 2-1 timu ya Morocco katika mchezo wa ufunguzi uliofanyika leo Novemba 27,2021 uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Timu ya Morocco ilianza kushinda goli la kwanza katika sekunde ya 18 ya mwanzo kupitia kwa mshambuliaji wake Chaamoun Redouane huku magoli ya Tanzania yakianza kufungwa kwenye dakika 15 kipindi cha pili na mshambuliaji Alfani Kiangi wakati bao la ushindi likishindiliwa na Nahodha wa Tembo Juma kidevu na kuifanya Tanzania kuibuka kidedea.

Hata hivyo timu ya Tanzania imekosa magoli mengi licha ya kuwa imeonesha kiwango kikubwa uwanjani ukilinganisha na Morocco.
Timu ya Tembo iliingia uwanjani ikiwa na ari kubwa huku ikishangiliwa na washabiki waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Uhuru hali iliyoonyesha wazi kuwa ushindi ni lazima.

Katika hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa alisisitiza kuwa timu ya Tembo inakwenda kufanya vizuri kutokana na maandalizi kabambe iliyofanya kwa usimamizi wa Serikali.
Awali, Novemba 25, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Waziri Mkuu aliitakia kila la kheri timu hiyo na kuizawadia shilingi Milioni 150 ilizisaidie maandalizi ya mashindano hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news