Wafanyakazi TAEC watoa tabasamu kwa watoto yatima na walemavu Kituo cha Mehayo

NA MWANDISHI MAALUM

WAFANYAKAZI wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) wameendelea kuwa mstari wa mbele kwa kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha wanarejesha tabasamu kwa makundi mbalimbali katika jamii yenye uhitaji maalum.
Wafanyakazi wa TAEC wakiwa katika kituo cha watoto yatima na walemavu walipokuwa wakitoa msaada wa chakula na madawa katika kituo cha Mehayo kilichopo Mazimbu mkoani Morogoro.(Picha zote na TAEC).

Katika kuhakikisha wanaondoka na baraka, wafanyakazi wa TAEC walifika katika kituo cha watoto yatima na walemavu cha Mehayo kilichopo Mazimbu mkoani Morogoro kutoa msaada wa chakula na madawa katika kituo hicho.
Ni kabla ya kuanza safari ya kurudi jijini Arusha baada ya hitimisho la Michezo ya
Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafasi Tanzania (SHIMMUTA).
Kwa nyakati tofauti, watoto katika kituo hicho walionekana wenye nyuso za tabasamu huku wakisikika wakisema, "Mungu awabariki wafanyakazi wa TAEC kwa msaada wao huo ambao ni muhimu sana katika kituo chao".

TAEC ni nini?

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ni taasisi ya Serikali iliyoundwa kwa Sheria ya Nguvu za Atomiki Na. 7 ya Mwaka 2003 (Atomic Energy Act No.7 of 2003) inayoipa TAEC mamlaka ya kudhibiti matumizi salama ya mionzi na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia nyuklia hapa nchini ili kulinda wafanyakazi, wananchi, wagonjwa na mazingira dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.
TAEC yenye Makao yake Makuu jijini Arusha ina Ofisi za Kanda na Mipaka zipatazo ishirini na saba (29), ambapo Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam ina jumla ya Ofisi ndogo ishirini na tatu (23), hii yote ni katika kuhakikisha udhibiti wa matumizi salama ya mionzi unafanyika kikamilifu sambamba na kuhakikisha TAEC inarahisisha ufanyikaji wa biashara kwa kutoa vyeti vya mionzi kwa wakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news