Tanzania yazidi kuboresha mazingira ya Uwekezaji

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SEKTA zilizopo chini ya Wizara ya Uwekezaji kikiwemo Kituo cha Huduma za Uwekezaji Nchini (TIC) imedhamiria kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Geoffrey Mwambe (aliyesimama) akieleza namna ya kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini ili kuongeza mapato yatakayosaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma.

Lengo likiwa ni kuongeza mapato yatakayosaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha anawaondolea kero wananchi wake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Geoffrey Mwambe ameyasema hayo katika katika kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa mifumo na wadau mbalimbali katika sekta ya uwekezaji.
Wataalamu wa mifumo na wadau mbalimbali katika sekta ya uwekezaji wakiwa katika kikao cha maazmio yenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wawekezaji ili taasisi zinazoshughulikia wawekezaji kuweka mfumo mzuri hivyo kupunguza msururu upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji hao.
Baadhi ya wajumbe wa sekta zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji ikiwemo Kituo cha Huduma za Uwekezaji nchini (TIC) wakifuatilia kwa makini mjadala uliokuwa ukiendelea juu ya kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini ili kuongeza mapato yatakayosaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma.

Kikao chenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wawekezaji hao, amesema mamlaka zote na taasisi zinazoshughulikia wawekezaji kuweka zinapaswa kuweka mfumo mzuri ili kupunguza msururu w upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji hao.

Naye Mkurugenzi Mtandaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.Maduhu Kazi amesema, mfumo huo utaweza kurahisisha kutoa huduma bora kwa wawekezaji.

Post a Comment

0 Comments