TANZIA: Mkufunzi wa Chuo cha DSJ, Joyce Mbogo afariki

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WANAFUNZI mbalimbali katika tansinia ya habari wameelezea kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha aliyekuwa mkufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ), Bi. Joyce Mbogo.
Mkufunzi huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa wanawake wachache waliokuwa wasikivu na wakarimu kwa wanafunzi wake alikuwa anafundisha chuo hicho chenye makao yake makuu eneo la Ilala Sharrif Shamba katika Halmashauri ya Jiji la Ilala, Dar es Saalam.

"Kifo cha Madam Joyi ni pigo kubwa sana katika tasnia ya habari, alikuwa dada mkarimu na msikivu ambaye ukiwa haujaelewa chochote kama mwanafunzi ukimfuata, atakuelekeza taratibu hadi uweze kuelewa, kwa kweli ni majonzi sana,"amesema mmoja wa wanafunzi hao.

Aidha, uongozi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) umethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

"Tumesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Madam Joyce Mbogo ambaye alikuwa Mkufunzi na mtaalamu wa kozi ya Public Relations and Advertising na Entrepreneurship hapa DSJ.

"Mchango wake katika jamii ya DSJ, taaluma ya Habari, Utangazaji, Uhusiano kwa Umma na Matangazo haitasahaulika kwakuwa ilisaidia kila mmoja kwa namna yake.Chuo cha DSJ, wafanyakazi na wanafunzi watamkumbuka daima kwa urafiki, ucheshi, ukarimu, usikivu, ushiriki wa Madam Joyce Mbogo katika matukio mbalimbali hapa DSJ.Mungu ailaze roho ya marehemu Joyce Mbogo, Amina,"imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na uongozi wa chuo Novemba 18, 2021.

Uongozi wa DIRAMAKINI BLOG unawapa pole wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao Joyce Mbogo. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.Amen.

Post a Comment

0 Comments