TARURA yaja na mfumo rafiki wa maegesho kidigitali, Wahariri, waandishi waelezwa utaanza Desemba Mosi,2021

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendesha semina elekezi ya kuwajengea uwezo Wahariri wa Vyombo vya Habari, Waandishi na Washawishi wa Mitandao ya Kijamii kuhusu Mfumo wa malipo ya Maegesho kwa njia ya Kielektroniki (TeRMIS) unaotarajiwa kuanza kutumika Desemba Mosi, 2021 katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Singida na Mwanza.
Kwa mujibu wa TARURA, Mtumiaji wa maegesho anapaswa kulipia Ushuru wa Maegesho Kidigitali baada ya kupatiwa namba ya malipo (control number) ambapo atatumia kumbukumbu namba hiyo kulipia maegesho kwa kutumia mtandao wowote wa simu ya mkononi, Benki ya NMB na CRDB au kupitia kwa Mawakala wa Huduma za fedha.

Pia mfumo huu wa Kidigitali unampa muda mtumiaji wa maegesho kulipia Ushuru wa Maegesho ndani ya Siku 14 tangu alipotumia Maegesho na endapo atashindwa kulipa ndani ya muda huo atatakiwa kulipa Ushuru wa Maegesho pamoja na faini ya Shilingi 10,000.
TARURA imeeleza kuwa, kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 500 kwa saa na Shilingi 2,500 kwa siku.

Aidha Mkoa wa Mwanza mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 500 kwa saa na Shilingi 1,500 kwa siku.

Kwa upande wa Mkoa wa Iringa mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa Saa na Shilingi 1,000 kwa siku.
Mkoa wa Dodoma mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa saa na Shilingi 1,000 kwa siku.

Hata hivyo, Mkoa wa Singida mtumiaji wa maegesho anatakiwa kulipa Shilingi 300 kwa saa na Shilingi 1,000 kwa siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news