Manchester United yajiandaa kuachia kichapo kwa Watford

NA MWANDISHI MAALUM

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema mashabiki wa timu hiyo wataona mabadiliko kiuchezaji kwenye timu hiyo kuanzia kwenye mechi ya leo Jumamosi Novemba 20,2021 dhidi ya Watford.
Ole Gunnar Solskjaer amesema hayo baada ya kikosi hicho kupitia wakati mgumu wa matokeo ikiwa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo katika mechi 12.

Baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, kocha huyo anasema, kila mmoja anaonekana mwenye ari kubwa.

“Wachezaji, viongozi, mimi mwenyewe na klabu inafanya kazi kwa ushirikiano kuhakikisha tunarudi kwenye njia zetu za ushindi,"amesema.

Post a Comment

0 Comments