Wabadilisha fikra za wanakijiji kutoka kuharibu misitu hadi uhifadhi kwa maendeleo

NA MWANDISHI MAALUM

MRADI wa Kuhifadhi Misitu kupitia Biashara Endelevu ya mazao ya misitu unaotekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) umewabadilisha wananchi wa Kijiji cha Nambinda wilayani Liwale mkoani Lindi na sasa wameacha tabia ya kuharibu misitu na wamejua thamani yake.
Wananchi wa Kijiji hicho wameanza kujua thamani ya misitu baada ya mashirika hayo kuwapa elimu ya ya shughuli za uzalishaji endelevu wa mazao yatokanayo na misitu na matumizi bora ya ardhi.

Mzalishaji wa mbao wa kijiji hicho Hemed Kipaga akizungumza kwa niaba ya wenzake wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu wilayani Liwale mkoani hapa waliotaka kujua hali ya utunzaji wa misitu ilivyokuwa kabla ya kupokea mradi huo alisema ilikuwa mbaya sana.
Mkuu wa Wilaya ya Liwale Judith Nguli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambao wapo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu wilayani Liwale mkoani Lindi katika mkutano uliofanyika jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Tina Sekambo akizungumza na waandishi wa habari.
Wajumbe wa Halmashauri ya kijiji hicho wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya waaandishi wa habari na maofisa kutoka mashirika ya TFCG na MJUMITA wakiwa kwenye mkutano huo.
Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG, Elida Fundi akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Uhusiano wa TFCG, Bettie Luwuge akizungumza katika mkutano huo.
Katibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji hicho, Saidi Barabara, akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Sadick Kiindi.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Saidi Kowe (kulia) akiwaonesha waandishi wa habari maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo ambayo yamekatwa miti. Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nambinda, Sadick Kiindi.
Katibu wa Kamati ya Maliasili ya Kijiji hicho, Saidi Barabara, akimkabidhi taarifa fupi ya mradi huo Afisa Uhusiano wa TFCG, Bettie Luwuge.
Afisa Mradi kutoka Shirika la TFCG, Peter Ibrahim akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Mlembwe, Mohamed Mahangabana akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Saidi Kowe akizungumza kwenye kikao hicho.

“Kwanza kabisa napenda kuyashukuru mashirika haya TFCG na MJUMITA kwa kutuletea mradi huu kwani tumeweza kufanikiwa mambo mengi, kabla ya mradi hatukuwa na matumizi bora ya ardhi ukataji wa miti ulikuwa wa ovyo ovyo tu mtu alipokuwa akijisia alikuwa akiingia msituni na kukata miti,” amesema Kipaga.

Amesema,baada ya kupata mradi huo wameweza kutenga maeeneo ya matumizi bora ya ardhi ambayo aliyataja kuwa ni ya makazi msongamano,eneo la kilimo na la kuhifadhi msitu na kuwa mpango huo umesaidia sana kuhifadhi misitu.

Awali akizungumza na waaandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale, Tina Sekambo alisema halmashauri hiyo imetenga sh.30 milioni kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa misitu na kuwa mabadiliko ya kiuchumi yamekuwa ni moja ya sababu ya wananchi katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo kukata miti ya asili na kuanza kupanda mikorosho.
Afisa Mistu wa Wilaya ya Liwale Lilian Kato (kulia) akimuelekeza jambo Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge wakati wa mkutano huo.
Rukia Timtim, akizungumza kwenye mkutano huo.
Amina Makanga, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mzalishaji wa mbao wa kijiji hicho, Hemed Kipaga akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja.

Mkuu wa Wilaya ya Liwale Judith Nguli alisema utunzaji wa miti ni jukumu la kila mwananchi na alitumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kufika katika wilaya hiyo kusaidia utunzaji wa misitu na kuwa mtu yeyote atakaye bainika akihalibu misitu kwa namna yoyote atachukuliwa hatua za kisheria.

Nguli aliyashukuru mashirika yanayoisaidia serikali katika suala zima la uhifadhi wa misitu ya asili katika wilaya hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news