Waziri Ali afanya uteuzi Shirika la Bima Zanzibar

NA GODFREY NNKO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mheshimiwa Jamal Kassim Ali ameteua wajumbe watano katika Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Bima Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mheshimiwa Jamal Kassim Ali. (NA MAKTABA).

Mheshimiwa Ali amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha cha 21 (1) (b) cha Sheria ya Msajili wa Hazina na Msimamizi wa Mali za Umma namba 6 ya 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 8, 2021 na Katibu Mkuu, Ofisi ya Raius, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Waziri amewateua wajumbe hao akiwemo;

Ndugu Ali Sultan Malik, Ndugu Bakari Rashid Bakari, Ndugu Hanifa Suleiman Hamza, Ndugu Mohamed Kassim Hassan na Ndugu Nahaat Mohammed Mahfouth.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, uteuzi huo umeanza Novemba 6, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news