Waziri Mchengerwa:Serikali na Benki ya Dunia itaendeleza ushirikiano wa kuzikwamua kaya maskini nchini

NA JAMES MWANAMYOTO, TEMEKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameiomba Benki ya Dunia kuendeleza ushirikiano uliopo wa kuzisaidia kaya maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwasababu umetoa matokeo chanya kwa kuboresha maisha ya kaya maskini nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wajasiriliamali wanaonufaika na TASAF wa Mtaa wa Nzasa A, Kata ya Kilungule, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Ujumbe wa Benki ya Dunia uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika mtaa huo.

Mhe. Mchengerwa ametoa ombi hilo wakati wa ziara ya kikazi ya ujumbe wa Benki ya Dunia uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mtaa wa Nzasa A, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mchengerwa amesema lazima Serikali ikiri kuwa TASAF haijasaidia tu kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja bali imesaidia kusogeza karibu huduma za kijamii kwa kujenga madaraja, shule na zahanati, hii yote ni kutaka Watanzania waondokane na umaskini unaosababishwa na maadui watatu ambao ni umaskini, ujinga na maradhi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Prof. Mari Pangestu wakiangalia bidhaa za wanufaika wa TASAF wa Mtaa wa Nzasa A, Kata ya Kilungule, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Ujumbe wa Benki ya Dunia uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika mtaa huo.

Mhe. Mchengerwa amesema, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kama ilivyokuwa kwa Serikali ya Awamu zilizopita ni kuumaliza umaskini kwa Watanzania na ndio maana imejipanga kuhakikisha watoto wanaotokana na kaya maskini ambao wamefaulu kujiunga na elimu ya juu wanapatiwa mikopo kwa asilimia mia moja ili elimu watakayoipata iwasaidie kupambana na umaskini.

Mhe. Mchengerwa amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia katika kupambana na umaskini na kuongeza kuwa TASAF itabakia kuwa ndio nyenzo mojawapo ya kuziinua kaya maskini nchini.

“Mhe. Mgeni Rasmi, tutaendelea kushirikiana katika kuboresha maisha ya Watanzania kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini ili kuondoa kaya maskini,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Prof. Mari Pangestu akizungumza na wajasiriliamali wanaonufaika na TASAF wa Mtaa wa Nzasa A, Kata ya Kilungule, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Ujumbe wa Benki ya Dunia uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika mtaa huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Prof. Mari Pangestu amesema ameona jinsi TASAF ilivyoboresha maisha ya Watanzania wengi wanaotokana na kaya maskini na kuongeza kuwa, ni dhahiri TASAF imepunguza kiwango cha umaskini nchini.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na wajasiriliamali wanaonufaika na TASAF wa Mtaa wa Nzasa A, Kata ya Kilungule, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Ujumbe wa Benki ya Dunia uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika mtaa huo.
Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Mtaa wa Nzasa A Kata ya Kilungule, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Prof. Mari Pangestu alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya Ujumbe wa Benki ya Dunia uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika mtaa huo.
Mnufaika wa Kikundi cha TASAF Vicoba Group cha Mtaa wa Nzasa A, Kata ya Kilungule, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Bibi Glory Paul akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kikundi hicho kwa Ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Sera za Maendeleo na Ubia wa Benki ya Dunia, Prof. Mari Pangestu wakati wa ziara ya kikazi ya ujumbe huo uliolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mtaa huo.

“Nikiwaangalia ninawaona mkiwa na afya njema, na ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kujali afya zenu ili muweze kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo,” Prof. Pangestu ameongeza.

Prof. Pangestu amemhakikishia Mhe. Mchengerwa kuwa, Benki ya Dunia itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika kupambana na umaskini kupitia Utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini unaoratibiwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news