Ziara ya Rais Samia nchini Misri yazidi kuangazia fursa zaidi

NA MWANDISHI MAALUM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Novemba 11, 2021 ameendelea na ziara yake ya Kiserikali katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa kutembelea mji mpya wa Serikali wa Cairo (New Cairo Administrative City).Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia ramani ya mji mpya wa kiserikali wa New Cairo Administrative City unaoendelea kujengwa Jijini Cairo nchini Misri, alipotembeleleo katika Makumbusho mapya yaliopo katika mji mpya wa Kiserikali Cairo Misri leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji saini Hati za makubaliano katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Biashara Huria nchini Misri Dkt. Mohammed Abdul-Wahabi leo tarehe 11 Novemba 2021 Jijini Cairo Misri. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Serikali ya Misri ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kuhamisha Makao Makuu ya Serikali katika mji mpya.

Katika mji huo mpya inatarajiwa Wizara, Taasisi za Serikali, Bunge, Mahakama, Balozi za nje zenye uwakilishi nchini Misri ikiwemo Tanzania na nyinginezo kuhamia kwenye eneo hilo ambalo pia litakapokamilika linatarajiwa kuwa na watu takribani milioni 6.5.

Aidha, Mhe. Rais Samia ametembelea eneo la viwanda la Kampuni ya Elsewedy ambao ni miongoni mwa wawekezaji wakubwa nchini Misri wanaokusudia kujenga eneo la uwekezaji viwanda nchini Tanzania. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia mabadilishano ya Hati za makubaliano katika Nyanja ya kukuza Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Biashara Huria nchini Misri Dkt. Mohammed Abdul-Wahabi leo tarehe 11 Novemba 2021 Jijini Cairo Misri. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa picha ya pamoja na Wafanyabiashara wa Misri baada ya kuzungumza na Wafanyabiashara hao leo tarehe 11 Novemba 2021Jijini Cairo nchini Misri, ambapo amewaelezea fursa mbalimbali za uwekezaji ziliopo nchini Tanzania. Mhe. Rais Samia yupo Nchini Misri akiendelea na ziara yake ya siku ya pili ya Kiserikali kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mji mpya wa New Cairo Administrative City Jijini Cairo nchini Misri leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea na ziara ya Kiserikali ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mji mpya wa New Cairo Administrative City Jijini Cairo nchini Misri leo tarehe 11 Novemba 2021. Mhe Rais Samia yupo Nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea na ziara ya Kiserikali ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.

Kampuni ya Elsewedy pia ndio mkandarasi mkuu wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere kwenye mto Rufiji.

Mhe. Rais Samia pia ametembelea Taasisi ya uwekezaji na biashara huria (General Authority for Investment and Free Zones) ambayo ni Mamlaka Maalum iliyo chini ya Wizara ya Uwekezaji yenye dhamana ya biashara na kutoa motisha maalum kwa wawekezaji kwenye maeneo husika na pia utoaji vibali vya biashara na uwekezaji nchini Misri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news