Azam FC yasaini kandarasi na kocha kutoka Marekani

NA MWANDISHI MAALUM

KLABU ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Abdihamid Moallin, kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha Kukuza Vipaji maarufu kama Azam FC Academy.
Moallin ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Somalia, alisaini mkataba mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim. 

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha Horseed ya Somalia, pia atakuwa akifanya uchambuzi wa mechi za timu kubwa ya Azam FC.

Pia amewahi kufanya kazi kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), katika timu ya Columbus Crew (2014-2016), kama Kocha Msaidizi wa timu hiyo na timu za vijana chini ya miaka 18 na 23 ikiwemo D.C United.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news