CCM yampongeza Rais Samia kwa ujenzi miundombinu ya kisasa nchini

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo kwa niaba ya chama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine.
Ameyasema hayo wakati akitoa salamu za CCM katika ziara maalum ya Rais Samia mkoa wa Dar es Salaam wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili Mkoa wa Dar es Salaam eneo la Mbagala Rangi tatu Desemba 4, 2021.
"Mheshimiwa Rais, Mbagala miaka miwili mitatu iliyopita, ilikuwa ukiona picha yoyote watu wananing'inia kwenye madirisha ya daladala ilikuwa wala hauulizi mara mbili unaambiwa hii Mbagala,lakini Mheshimiwa Rais umefanya uamuzi mkubwa wa kuhakikisha awamu ya pili ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka yanakuja kutatua changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili wananachi wa Mbagala,"amesema.

"Kwa kweli katika jiji hili la Dar es Salaam Mbagala ni miongoni mwa maeneo yenye idadi kubwa ya wananchi hivyo Mheshimiwa kwa niaba ya chama ninakupongeza sana kwa uamuzi huu wenye tija," Katibu Mkuu ameongeza.

Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa, "Ujenzi wa miundombinu hii ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ambapo kwenye ukarasa wa 71-78 ndipo kuna ahadi ya kuhakikisha tunasogeza mindombinu bora na yenye kurahisisha usafiri kwa wananchi wetu ndani ya jiji hili la Dar es salaam,"amesema.

Awali, Katibu Mkuu ameshiriki pia, ziara ya Mheshimiwa Rais katika eneo la Bandari ambapo umefanyika uzinduzi wa Magati ikiwa ni muendelezo wa utanuzi wa miundombinu ya bandari na uboreshaji wa huduma za bandari ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM fungu la 59.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news