Idris Sultan awa Mtanzania wa kwanza kwenda kusherehesha Tuzo za AEAUSA nchini Marekani

NA GODFREY NNKO

MTANZANIA ambaye ni mshindi wa Big Brother Africa ‘Hotshots’ mwaka 2014, Idris Sultan ambaye pia ni muigizaji nchini Tanzania ametangazwa rasmi kama mshereheshaji katika Tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) zinazotarajiwa kufanyika Desemba 26, 2021 nchini Marekani.
Miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania ambao wanawania tuzo hizo ni pamoja na Mfalme wa Bongo Fleva,Ali Kiba, Staa wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz,Harmonize,RosaRee, Rayvanny, Zuchu, Mbosso, MimiMars, Nandy Weusi na MacVoice.

Idris Sultan kwa kushirikiana na mshereheshaji Nancy Isime ndiyo wanatarajiwa kuonyesha vipaji vyao katika kufanikisha mashindano hayo ya saba ya AEAUSA.

Huu ni mwendelezo wa mafanikio ya Mtanzania Idris Sultan katika kuiwakilisha Tanzania kwenye anga za Kimataifa ikiwa ni hivi karibuni tu alianza kuonekana katika mtandao wa Netflix.

Alikuwa ni Mtanzania wa kwanza, kuanza kuonekana katika mtandao wa Netflix ambayo ni huduma namba moja duniani inayoonyesha video za filamu na tamthilia kwa njia ya kuzitazama kupitia huduma ya intaneti maarufu kama ‘streaming’.

Mafanikio hayo yalianza Aprili 27, 2021 ambapo Netflix walianza kuionesha filamu ya ‘Slay’ ambayo mwigizaji huyo wa Kitanzania ameshiriki akiwa ameigiza kama kijana tajiri anayetafuta mwanamke mwenye mapenzi ya kweli ili kufikia ndoto zake.
Uongozi wa DIRAMAKINI BLOG unamtakia Idirs Sultan na Watanzania wote ambao wameonyesha bidii ya kutumia vipaji vyao kuiwakilisha Tanzania katika anga za Kimataifa mafanikio mema, pia unawatakia washiriki wote ushindi mwema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news