Kesi dhidi ya Paul Makonda yafutwa na MAHAKAMA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni mkoani Dar es Salaam imetupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda kutokana na mapungufu ya kisheria.
Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 3,2021 na Hakimu Allon Lyamuya baada ya upande wa mleta maombi, Saed Kubenea kupitia Wakili wake, Hekima Mwasipu kuomba kuiondoa kesi hiyo kutokana na kukosea baadhi ya sheria wakati wa kuifungua.

Kutokana na hatua hiyo, Wakili Mwasipu amesema wataifungua kesi hiyo tena baada ya kumaliza marekebisho ya vifungu vya sheria ambavyo hakuvitaja.

"Lengo la kuiondoa ni kufanya maboresho kwa sababu ni kesi yenye maslahi mapana kwa taifa, tumepokea maoni kutoka kwa Wadau, nadhani hadi Jumatatu inaweza kuwa tayari,” amesema Wakili Hekima.

Mheshimiwa Said Kubenea kupitia wakili wake Mwasipu, alimshitaki Paul Makonda katika kesi ya jinai namba 7 ya mwaka 2021 katika tuhuma mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, mbali na Makonda washitakiwa wengine walikuwa ni Mkurugenzi wa Mashitaka na DCI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news