Miaka 60 ya Uhuru: Viongozi Mkoa wa Singida wabisha hodi maeneo ya kihistoria

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAKAZI wa Mkoa wa Singida wametakiwa kujenga tabia ya kuyatembelea maeneo ya historia na kijifunza historia ya mkoa wao na nchi yao kwa ujumla ili waweze kutambua walivyokuwa wakiishi watu wa maeneo hayo kabla na baada ya Uhuru.

Imebainika kwamba ili kujua hatua ambazo nchi imeweza kupiga na kuleta maendeleo ya uchumi, siasa na utamaduni ni lazima kuijua historia ya zamani ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo Desemba 5, 2021 na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya kihistoria yakiwemo Ofisi ya DC wa kwanza Mwafrika iliyopo Manyoni mkoani Singida, Nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la Mjini Kati Manyoni, vituo mbalimbli vya kihistoria eneo la Kilimatinde na reli ya mwendokasi iliyopo Makutopora ambapo alibanisha umuhimu wa kujifunza historia ya maeneo hayo.

Ziara hiyo ilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru ambayo Mkoa wa Singida unaendelea kuadhimisha kwa namna tofauti mpaka itakapofika Desemba 8 mwaka huu kabla ya kuungana na maadhimisho ya kitaifa yatakayofanyika tarehe 9 katika uwanja wa Uhuru mkoani Dar es salaam.

Mwaluko amefafanua kwamba, pamoja na historia lakini wananchi wa Mkoa wa Singida wanapaswa kufahamu jitihada za Serikali katika kuliletea taifa maendeleo kwa kuanzisha reli ya mwendo kasi ambayo imesemekana itarahisisha usafiri na kuongeza biashara maeneo mbalimbali.
Ziara hiyo ilihusisha wakurungezi wa Halmashauri saba za Mkoa wa Singida, Wakuu wa Wilaya ya Singida Mjini na Iramba pamoja na wabunge mbalimbali lengo likiwa ni kuwaonesha wananchi fursa nyingine za kiutalii ambazo huweza kulisaidia taifa kupata mapato kupitia vitu vya kihistoria.

Naye DC wa Singida,Mjini Mhandisi Pasikas Muragili akimwakilisha DC wa Manyoni akatumia muda huo kuwataka Vijana kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo kwa kuwa yana mafunzo ndani yake.

DC Muragili akawataka pia vijina kujitokeza siku ya tarehe sita katika ukumbi wa mikutano wa Halamashauri ya wialaya ya Manyoni kushiriki kongamano juu ya hatua mbalimbali zilizofikiwa na Serikali kabala na baada ya uhuru.

Amesema katika kongamano hilo litakuwa na mada mbalimbali ambazo zitasaidia kueleza wapi tulipotoka, tupo wapi na muelekeo ni upi katika nyanja za afya elimu uchumi na mengine kama hayo.

Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Manyoni Abubakari Mange Kisunda anabainisha kwamba eneo la kilimatinde lilipata umaarufu zaidi wakati wa vita vya wahehe na makabila mengine ambapo viliweza kuishia hapo kwa kuwekewa mtego na wenyeji wa bonde la ufaa na uliwafanya kurudi nyuma.

Abubakari ameendelea kusema kwamba Kilimatinde ilikuwa ni kitovu cha kupitisha wageni toka nchi za nje ambapo ilitumika kama kituo cha kupumzikia.
Aidha, wageni wengi walikuwa wakipita na misafara yao ya biashara mbalimbali zikiwemo biashara za watumwa ambazo ziliwahusisha waarabu,waajemi , Wapelelezi na walowezi walifika maeneo haya wakitokea pwani kwenda bara aliafafanua Afisa Biashara.

Aidha alibainisha kwamba Wafanya biashara walitaka kupata pembe za ndovu, Ngozi za wanyama kama chui na simba kwa Kubadilishana na shanga, nguo na watumwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news