Udaktari wa Heshima katika siasa na uongozi wa Mbunge Musukuma

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBUNGE wa Geita Mjini, Joseph Kasheku maarufu kama Msukuma ametunukiwa Udaktari wa Heshima katika siasa na uongozi (Honoris Causa in Politics and Leadership) na Chuo cha Academy of Universal Global Peace cha Marekani.

Heshima hiyo ni kama sehemu ya kutambua mchango wake kwenye siasa na uongozi nchini Tanzania.

Sherehe za kutunukiwa udaktari huo wa heshima zimefanyika jijini Dododma, Desemba 5,2021.

Hata hivyo, Academy of Universal Global Peace kilichompa heshima hiyo, Mheshimiwa Mbunge Musukuma makao yake makuu yapo nchini India.
Tovuti yake inaeleza kimesajiliwa India, Uingereza na Marekani, ingawa hakipo katika tovuti rasmi za taifa za vyuo vya Uingereza na Marekani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news