Pwani yatamba michuano ya Samia Taifa Cup

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TIMU za Mkoa wa Pwani za Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete zimetamba baada ya kupata ushindi dhidi ya washindani wao kwenye michuano ya Samia Taifa Cup.
Michezo hiyo ambayo inatimua vumbi jijini Dar es Salaam ambapo ilianza juzi Pwani walionyesha umahiri mkubwa.

Kwenye mchezo wa soka Pwani iliwatambia wenyeji kwa kuwanyuka kwa magoli 3-2 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Duce.

Upande wa mchezo wa mpira wa Pete Pwani ilitamba kwa kuifunga Geita kwa magoli 52-31.

Meneja wa timu ya soka ya Pwani, Simon Mbelwa amesema kuwa kutokana na ushindi huo anaamini vijana wake watafanya vizuri kwenye mchezo ujao.

Mbelwa amesema, mchezo wao utakaofuata watachuana na Kaskazini Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news