Rais Dkt.Mwinyi atoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Mzee Haji Mkombe Ame

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Mzee Haji Mkombe Ame aliyefariki juzi na kuzikwa Desemba 6,2021 huko kijijini kwao Bambi ya Bondeni Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na kifo cha marehemu Mzee Haji Mkombe Ame ambaye alikuwa Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Zanzibar na kuiomba familia kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Haji Mkombe Ame mahala pema peponi, Amin.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news