Rai hiyo ameitoa Desemba 2, 2021katika ufunguzi wa Kituo cha Kulea Watoto cha pamoja cha huduma ya mkono kwa mkono kwa watoto waliofanyiwa ukatili kilichopo Chuo Kikuu Kishiriki cha SAUT, Jordan kilichopo Morogoro.Amesema, kwa takwimu za Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali huduma dhidi ya ukatili kwa watoto imeendelea kutoa huduma katika vituo 17 vya mkono kwa mkono hapa nchini na katika kipindi cha Julai 2020 hadi juni 2021 kulikuwa na waathirika 1,857 wa kufanyiwa ukatili wa kijinsia na kati yao watoto 1,072 walihudumiwa.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Martine Shigela akimkaribisha Waziri wa Afya, Dkt.Gwajima amesema kuwa, Mkoa wa morogoro unakabiliwa na changamoto ya uwepo wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo Jeshi la Polisi kwa Julai hadi Septemba 2021 limepokea taarifa za unyanyasaji wa kijinsia kwa watu wazima 200 kati yao wanaume wapo 41 na wanawake 159 huku taarifa za watoto 275 zikitajwa kati yao 64 ni wavulana na watoto 136 watoto wa kike.Hali inayoonyesha watoto wa kike na wakina mama kuwa kwenye mazingira magumu kiasi cha kuhitaji kuimarisha kamati ya ulinzi na usalama ziweze kuweka mikakati madhubuti ili kukabiliana na hali hiyo.
Mkuu wa Chuo Kishiriki cha Jordan, Prof.Bertram Mapunda amesema kuwa chuo kimebaini Morogoro ukatili upo kwa kiwango cha asilimia 60 ambapo kila watoto 10 sita hufanyiwa ukatili wa aina mbalimbali ikiwemo ulawiti,ubakaji,vipigo,kuunguzwa kwa maji na moto watoto pindi wanapokosea,kuwafanyisha kazi ngumu,kuwanyima chakula,haki ya kupata elimu,matibabu na malezi bora kutokana na ugomvi wa wazazi,ulevi uliopindukia na msongo wa mawazo hali inayohatarisha maisha ya watoto wadogo