WAZIRI MCHENGERWA AELEKEZA WALENGWA WA TASAF KUPEWA RUZUKU KABLA YA KRISMASI ILI WAJIPANGE KUBORESHA MAISHA YAO

NA JAMES K.MWANAMYOTO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Waratibu wa TASAF nchini kuhakikisha walengwa wanapewa ruzuku kabla ya Sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya ili waweze kujipanga mapema kuboresha maisha yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akicheza ngoma na wasanii wa kikundi cha Mapigo Tisa cha Kazuramimba mara baada ya kuwasili Kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na walengwa wa TASAF akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

Akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Waziri Mchengerwa amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alishatoa maelekezo ya kuwapatia ruzuku walengwa wa TASAF mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uandikishaji na uhakiki.

“Waratibu wa TASAF hakikisheni walengwa wa Kazuramimba wanalipwa kwa wakati kabla ya Krismasi ili wapange mikakati madhubuti itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi katika Mwaka Mpya unaokuja,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kigoma.

Akizungumzia azma ya Serikali ya kuwahudumia wananchi, Mhe. Mchengerwa amesema, Serikali isiyowajali walengwa wa TASAF ni sawa na Serikali isiyokuwa na huruma kwa wananchi wake na kukosa hofu ya Mwenyezi Mungu.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, dhamira ya Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kuzifikia kaya milioni moja na laki tano ambazo ni sawa na Watanzania milioni kumi na tano ambao watanufaika na mpango wa kuzinusuru kaya zenye uhitaji.
Baadhi ya wananchi na walengwa wa TASAF wa Kijiji cha Kazuramimba wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Kijiji hicho Mkoani wa Kigoma.

Waziri Mchengerwa amesema, Baba wa Taifa alisema kama Taifa hatutaweza kupiga hatua iwapo Watanzania wengi wana hali duni ya maisha na ndio maana Serikali ya Awamu ya Sita imeamua kuzikwamua kaya zisizojiweza kupitia mpango wa TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi Mhe.Thobias Andengenye akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kuzungumza na wananchi wa Kazuramimba wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Kigoma.

Katika kuhakikisha miradi ya TASAF inatekelezwa ipasavyo, Mhe. Mchengerwa amesema akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya kumsaidia Mhe. Rais kusimamia utekelezaji wa miradi ya TASAF, atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kutimiza azma ya Mhe. Rais kuzifikia kaya zote zenye hali duni nchini.

Mhe. Mchengerwa amehitimisha ziara ya kikazi mkoani Kigoma yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akielekea kukagua miradi ya TASAF iliyopo Kijiji cha Kazuramimba, akiwa na viongozi, watendaji na baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Kigoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akisikiliza ushuhuda wa mlengwa wa TASAF, Bi. Hija Kaziyabure wa Kijiji cha Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Mkoani Kigoma. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akimpongeza mlengwa wa TASAF, Bi. Tamasha Zegeli wa Kijiji cha Kazuramimba, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kwa matumizi mazuri ya ruzuku ya TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Mkoa wa Kigoma.

Post a Comment

0 Comments