Soma habari zote muhimu leo Oktoba 31, 2026 kutoka katika magazeti makubwa ya Tanzania kama Mwananchi, HabariLeo, Nipashe, Zanzibar Leo, Majira, Mwanaspoti, Uhuru na mengineyo kila siku bila malipo.
NIPASHE - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Nipashe leo habari kuu ni ‘Ndoto imetimia’ ambapo adhama ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere ya mwaka 1973 imetekelezwa kwa kuwa na mji wa serikali wenye majengo ya kisasa na Rais Samia atoa maelekezo wakati akiwa na Rais wa Angola João Lourenço kuzindua barabara za Jiji la Mtumba, likiandika pia Zungu acharuka matumizi ya ‘V8’ na kuagiza uchunguzi, watoto 400 kati ya 700 wabainika kuwa na msongo wa mawazo Dar na watatu mbaroni kwa tuhuma ya kumtorosha mwanafunzi wa sekondari.
Nipashe michezo leo habari kuu ni sababu Simba SC kutaabika Manyara, na Ramovic ‘live’ Yanga ikiikaribisha Kagera Sugar.
WAMACHINGA - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Wamachinga leo habari kuu ni Samia: Nimetimiza ndoto ya Nyerere ambapo asema Serikali imejenga Mji wa Mtumba kwa fedha za Watanzania hakuna shilingi ya mkopo, awataka watumishi kutumia mazingira bora kuwahudumia wananchi kwa heshima, uadilifu na ufanisi kwa mifumo kusomana na Rais Joao Lourenco wa Angola amwaga sifa Tanzania kwa kasi ya maendeleo, likiandika pia Mwigulu ataka Ubalozi Urusi kupanua masoko bidhaa za Tanzania, Mwinyi avutia wawekezaji Korea miradi ya mabilioni, watatu watiwa mbaroni tuhuma za utekaji, DC Shaka: Dkt Samia amewaibisha waliobeza na Spika Zungu aagiza maofisa walionunua mashangingi wahojiwe.
Wamachinga Spoti leo habari kuu ni Nkwabi atajwa kuwania Mwenyekiti Simba na Samsoni Adam Katibu Mkuu CAF, likiandika pia Lukindo azidi kuipaisha Namungo, Gary Neville ataka Man U kuuzwa na AFCON kuchezwa baada ya miaka miwili.
MWANA HABARI - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Mwana Habari leo habari kuu ni Dkt Samia ataka mji wa Serikali kurahisisha huduma kwa wananchi ambapo ni wakati akizindua ofisi na miundombinu yake Dodoma na awataka watumishi kuzingatia sheria na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yao, likiandika pia mkuu wa Wilaya Ludewa awataka viongozi kuwa mabalozi wa elimu ya fedha nchini, Dkt Mwinyi akutana na makampuni ya Korea ajadili fursa za uwekezaji miradi mikubwa Zanzibar, watatu mbaroni Moro kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha nne na Dkt Mwigulu awataka watumishi Ubalozi wa Tanzania Urusi waendelee kuitangaza vyema nchi.
Mwana Habari michezo leo habari kuu ni Kagoma: Fountain hali ya hewa haikuwa nzuri, likiandika pia Samson katibu mkuu mpya CAF, CAF: AFCON kuchezwa baada ya miaka miwili, Yanga yamtangaza Kocha Ramovic na Mbwana awakabili PSG League 1.
MTANZANIA LEO - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Mtanzania Leo leo habari kuu ni Ndoto imetimia ambapo Rais Samia akamilisha ndoto za Mwalimu Nyerere, azindua majengo ya serikali mji mpya wa Mtumba na asisitiza mifumo ya serikali isomane, likiandika pia DC Ludewa ataka elimu ya fedha, mama lishe, boda boda wampongeza Rais Dk Samia, Dk Mwigulu ataka ubalozi Urusi upanue soko bidhaa za Tanzania na Tanzania yapokea uenyekiti Baraza la Mawaziri ziwa Tanganyika.
BIASHARA LEO - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Biashara Leo leo habari kuu ni Rais Samia atimiza ndoto za Mwalimu Nyerere ambapo azindua majengo ya serikali mji mpya wa Mtumba, asisitiza mifumo ya serikali isomane, mama lishe, boda boda, wananchi wampongeza na ni kwa kufanikisha serikali kuhamia Dodoma, likiandika pia Tanzania yapokea uenyekiti Baraza la Mawaziri ziwa Tanganyika.
RAIA MZALENDO - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Raia Mzalendo leo habari kuu ni Rais Samia aandika historia nyingine ambapo akamilisha na kuzindua majengo ya serikali Mtumba, asisitiza mifumo ya serikali isomane kurahisisha huduma na ataka watumishi watumie fursa hiyo kutoa huduma bora, likiandika pia Rais Mwinyi akutana na kampuni za Korea, mkuu wa wilaya ya Ludewa awataka viongozi kuwa mabalozi wa elimu ya fedha na Masauni apokea uenyekiti Baraza la Mawaziri ya Ziwa Tanganyika.
MWANANCHI - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Mwananchi leo habari kuu ni safari ya historia ambapo ndoto ya miaka 53 ya kuifanya Dodoma makao makuu ya Serikali yatimia yaingia kwenye rekodi za nchi ya tatu Afrika hizi ndio falda za Mji wa Mtumba kwa Serikali, wananchi na Rais Samia ataka ufanisi, uwajibikaji huku akionya Rais Lourenco alivyookunwa na Mji wa Mtumba, likiandika pia Mahakama Kuu yaamuru Mwaipaya apelekwe akiwa hai au amekufa na Starehe Niffer ni Amina Chifupa wa kizazi hiki.
MWANA SPOTI - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Mwana Spoti leo habari kuu ni rekodi kali ambapo Simba SC yaifunika Yanga SC huku Barker aitupia jicho Berkane na ni mechi 9 za mwisho TPL ambapo ushindi 9, sare 0, kupoteza 0, likiandika pia Derby Day! Orlando Pirates vs Kaizer Chiefs, Bayern Munich vs Dortmund, AC Milan vs Inter Milan, EPL Pamoja Chelsea vs Man United, Man City vs Brighton, Tottenham vs Crystal Palace, Carrick 'Mfu' anayetembea, Ronaldo bado 15 baada ya kufunga bao la 5-2 Al Nassr na kibano makocha 6 Bara.
HABARI LEO - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Habari Leo leo habari kuu ni kishindo cha Rais Dk Samia Dodoma ambapo atimiza maono ya Nyerere akikamilisha Mji wa Serikali, akataa urasimu, ujenzi holela na ataka huduma zisogezwe kwa wananchi huku Rais Lourenco akiita Watanzania ubia wa madini, mafuta na gesi, likiandika pia reli kuunganisha nchi za Tanzania, Zambia, Angola, Zungu akerwa na magari ya anasa serikalini na watu 3 mbaroni mmoja asakwa tuhuma ya kuteka na kutorosha mwanafunzi.
Habari Leo michezo habari kuu ni Barker achekelea pointi tatu muhimu ambapo kocha mkuu wa Simba Steve Barker amesema muhimu timu hiyo kuondoka na pointi tatu bila kujali wamecheza vipi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Tanzania Kwaraa, likiandika pia Azam FC kuikabili JKT, Coastal wenyeji wa Dodoma Jiji, Olise aponda wachezaji Nigeria na Serengeti Boys yaahidi makubwa Qatar.
UHURU - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Uhuru leo habari kuu ni historia yaandikwa ni baada ya Rais Dk. Samia kuzindua Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma huku akiwasisitiza watumishi wa umma kuhudumia wananchi kwa heshima na uadilifu mkubwa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais Joao Lourenco wa Jamhuri ya Angola wakizindua barabara za lami, majengo ya ofisi za wizara na taasisi katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, likiandika pia Tanzania yapokea kijiti uenyekiti Ziwa Tanganyika, wachumi waanika faida zake na Zungu aagiza uchunguzi walionunua mashangingi.
Uhuru Michezo leo habari kuu ni Barker ang'aka huku Tanzania mguu sawa AFCON, likiandika pia TFF yatolea macho soka la wanawake, Tara aizima Man City, Russo apiga hat trick na Yanga waleteni Kagera Sugar muone.
TAIFA TANZANIA - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Taifa Tanzania leo habari kuu ni mji wa serikali kuwa mfano wa kutunza mazingira ambapo Rais Dk. Samia aelekeza muda wote wa mwaka uwe kijani wakati akizindua barabara za Mtumba, likiandika pia mbunge aomba sheria ya kuwahasi wanaobaka na kulawiti watoto, mkuu wa Wilaya Ludewa awataka viongozi kuwa mabalozi wa elimu ya fedha nchini na serikali kupiga marufuku pombe kali kulinda afya za Watanzania.
Michezo leo habari kuu ni CAF yarejesha AFCON kila baada ya miaka miwili ambapo wadau wapigia kilele ongezeko la timu, likiandika pia Ibrahim Class apima uzito akisema sala zenu tu mkanda ubakie nyumbani, wazee wa Simba SC watishia kwenda mahakamani kupinga uamuzi mkuu na Dodoma Jiji yajipanga kukabiliana na Coastal Union leo.
ZANZIBAR LEO - Jumamosi Oktoba 31, 2026
Gazeti la Zanzibar Leo leo habari kuu ni Dk. Mwinyi azikaribisha kampuni za Korea kuwekeza Zanzibar huku akibainisha maeneo na sekta za miradi ya kimkakati wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kampuni mbali mbili za Korea Kusini zilizoonyesha nia ya kuwekeza nchini, likiandika pia Amani ndio msingi wa maendeleo Tanzania - Hemed, Mtumba ufanane na mazingira ya Mji Mkuu - Dk. Samia na Zanzibar kujifunza uzoefu wa wanawake wa Jeju - Mama Mariam.
AN NUUR - Oktoba 30, 2026
Gazeti la An-Nuur leo habari kuu ni Mwigulu kuongoza harambee ya ujenzi wa Shule ya Kiislam ya Uchira Novemba 25 huku Dr. Alhad akiwaita wadau, likiandika pia Tusimame na Tanzania yetu ambapo Sheikh Mtupa akilaani chokochoko na kuwataka vijana kuwa makini na propaganda, na Tukumbuke Mauaji ya Waislamu Mwembechai 1998 na mauaji ya raia Zanzibar 2000 na 2001.
KIONGOZI - Oktoba 30-Nov 05, 2026
Gazeti la Kiongozi leo habari kuu ni ‘Tutubu, tuache kiburi, tujenge Taifa lenye Amani’ Pd. Kitima huku Askofu wa Jimbo Katoliki Njombe Mhashamu Eusebio Kyando akimtunuku Cheti Cha Pongezi Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Ovolanus Thomas kama mmoja wa wahitimu wa Jubilee ya Miaka 25 ya Parokia ya Ludewa Jimbo Katoliki Njombe, likiandika pia ‘Usipende kusifiwa na mwanadamu, msikilize Mungu’ Ask. Kinyaiya na ‘Mauaji, Ukatili vinatishia Ustawi wa Jamii’ Ask. Msonganzila.
TUMAINI LETU - Ijumaa Oktoba 30 hadi Novemba 5, 2026
Gazeti la Tumaini Letu leo habari kuu ni kumbukumbu vurugu za Oktoba 29, 2025 ambapo kanisa latoa ujumbe mzito, likiandika pia katika makala ya Saikolojia: Wanawake hujali urembo kuliko wanaume, Yanga yaipiku Simba kubadili makocha, Askofu Kinyaiya ampa neno Askofu Mpwaji na Askofu Ruwa'ichi: Acheni Injili ya bei poa isiyo na msalaba.




















