Waziri Ummy aagiza mkuu wa shule kushushwa cheo

NA NTEGHENJWA HOSSEAH,OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora kumshusha cheo cha ukuu wa shule, Mwalimu Nicolous Magwendela aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Makazi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora.
Mhe. Ummy ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake wilayani humo ambapo alipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa viongozi wa wilaya hiyo kuhusiana na Mwalimu huyo na kuelekeza ufuatiliaji wa haraka.

Baada ya kujiridhisha na mwenendo usiofaa wa utendaji kazi wa Mwalimu huyo, Waziri Ummy alielekeza hatua za haraka zichukuliwe ikiwemo kumtoa katika nafasi ya ukuu wa shule.

Wakati huo huo, Waziri Mhe.Ummy amewataka walimu wote nchini kufanya kazi kwa kuzingatia miiko ya kazi yao.

Post a Comment

0 Comments