Waziri Mchengerwa atoa wiki mbili kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wanaoishi mjini kuhamia maeneo wanayofanyia kazi

NA JAMES K.MWANAMYOTO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Rosemary Senyamule kusimamia maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ya kuhakikisha Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wanaoishi Geita mjini kuhamia maeneo ya jirani na vituo vyao vya kazi ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi waliofuata huduma za afya kwenye zahanati ya Kakubilo, iliyojengwa na TASAF wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo hayo katika Kijiji cha Kakubilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

Mhe. Mchengerwa amesema, Mhe. Waziri Mkuu alikwishatoa maelekezo ya watumishi wote wanaofanya kazi Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuishi katika vituo vyao vya kazi lakini bado kuna watumishi wanaishi Geita mjini jambo ambalo linaathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kakubilo na watumishi wa zahanati ya Kakubilo Mkoani Geita kabla ya kukagua zahanati ya kakubilo iliyojengwa na TASAF kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

“Pamoja na maelekezo aliyoyatoa Mhe. Waziri Mkuu, lakini nimepata taarifa kuwa kuna watumishi bado wanaishi Geita mjini na sio kwenye vituo vyao vya kazi huku wakitumia gharama za Serikali kuwafikisha kwenye vituo vyao vya kazi kila siku,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Katika kuhakikisha maelekezo ya Waziri Mkuu yanatekelezwa kikamilifu, Mhe. Mchengerwa ametoa wiki mbili kwa watumishi wote wa halmashauri hiyo wanaoishi Geita mjini kuhamishia makazi yao kwenye maeneo wanayofanyia kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwasili katika Kijiji cha Kakubilo Mkoani Geita kukagua Zahanati iliyojengwa na TASAF kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kakubilo mkoani Geita wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, anatarajia ndani ya wiki mbili alizozitoa, watumishi wote wanaoishi mjini watakuwa wamehamia karibu na maeneo wanayotoa huduma kwa wananchi na kwa kuwa ana vyanzo vingi vya kupata taarifa, hatosita kuchukua hatua kwa watakaokaidi.

Mhe. Mchengerewa amesema yeye ni mlezi wa Watumishi wa Umma, hivyo amelazimika kwenda Wilayani Geita ili kuhakikisha maelekezo ya Waziri Mkuu yanatekelezwa kwa manufaa ya wananchi.
Baadhi ya watumishi wa Zahanati ya Kakubilo mkoani Geita wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Geita.

Aidha, Waziri Mchengerwa amekagua zahanati ya Kakubilo iliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF na kuwaahidi wananchi wa Kijiji hicho kuwa ofisi yake itahakikisha inapeleka watumishi watakaotosheleza kutoa huduma kwa wananchi.

Mhe. Mchengerwa amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Geita kwa kuhimiza watumishi kuishi katika maeneo wanayofanyia kazi ili waweze kuwa na tija katika utoaji wa huduma kwa umma.

Post a Comment

0 Comments